159 Ubinadamu wa Kristo Waelekezwa na Uungu wa Mungu

1 Ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake. Ingawa yuko katika mwili, ubinadamu Wake si kama ule wa binadamu wa mwili kabisa. Anao upekee wa tabia Yake Mwenyewe, na hii pia huongozwa na uungu Wake. Uungu Wake hauna udhaifu; udhaifu wa Kristo unaelezea ule wa ubinadamu Wake. Kwa kiasi fulani, udhaifu huu huzuia uungu Wake, lakini mipaka hiyo ipo tu kati ya wigo fulani na wakati, na sio zisizo na mipaka. Linapokuja suala la muda wa kufanya kazi ya uungu Wake, hufanyika bila kujali ubinadamu Wake. Ubinadamu wa Kristo kabisa huongozwa na uungu Wake. Mbali na maisha ya kawaida ya ubinadamu Wake, matendo mengine yote ya ubinadamu Wake ni ya kushawishiwa, inayoathirika na kuelekezwa na uungu Wake.

2 Ingawa Kristo Anao ubinadamu, haukatizi kazi ya uungu Wake. Hii hasa ni kwa sababu ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake; ingawa ubinadamu Wake haujakomaa katika mwenendo Wake mbele ya wengine, hauathiri kazi ya kawaida ya uungu Wake. Ninaposema kwamba ubinadamu Wake haujapotoshwa, Ninamaanisha kwamba ubinadamu wa Kristo unaweza moja kwa moja kuongozwa na uungu Wake, na kwamba Yeye ni mwenye hisia kubwa kuliko ile ya mwanadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake unafaa zaidi kwa kuongozwa na uungu katika kazi Yake; ubinadamu Wake una uwezo wa kuonyesha kazi ya uungu, kama vile unao uwezo wa kutii kazi kama hiyo. Mungu Anapofanya kazi katika mwili, hajawahi kamwe kupoteza maono ya wajibu wa mwanadamu katika mwili Anaopaswa kutimiza; Anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli. Anayo dutu ya Mungu, na utambulisho Wake ni mfano wa Mungu Mwenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 158 Mbinu na Kanuni ya Kazi ya Mungu kwa Wanadamu

Inayofuata: 160 Jinsi ya Kumjua Mungu wa Vitendo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp