176 Mungu Alikuwa Mwili Kufanya Kazi kwa Ajili ya Mwanadamu

1 Sababu pekee ambayo Mungu mwenye mwili amefanyika mwili ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu aliyepotoka. Ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu na si ya Mungu, na mateso Yake na sadaka ni kwa ajili ya mwanadamu na si kwa manufaa ya Mungu Mwenyewe. Hakuna faida wala hasara au tuzo kwa Mungu; Hatavuna mavuno yoyote ya baadaye, bali ni kile ambacho hapo awali Aliwiwa. Yote Anayoyafanya na kujitolea kwa ajili mwanadamu si kwa sababu Atapata thawabu kubwa, bali ni kwa ajili ya mwanadamu. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inahusisha ugumu mwingi usiofikirika, matokeo ambayo yanapatikana mwishowe yanazidi kwa mbali sana kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja.

2 Kazi ya mwili inahusisha taabu nyingi sana, na mwili hauwezi kuwa na utambulisho mkubwa kama wa Roho, hauwezi kufanya matendo ya kimiujiza kama Roho, sembuse kuwa na mamlaka kama ya Roho. Lakini kiini cha kazi inayofanywa na mwili huu usiokuwa wa kawaida ni kuu zaidi kulinganisha na kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na mwili huu Mwenyewe ndio jibu kwa mahitaji yote ya wanadamu wote. Kwa kuwa kila mtu anayetafuta ukweli na anatamani kumwona Mungu, Kazi ya Roho inaweza kutoa tu kuguswa au msukumo, na hisia ya kuona maajabu ambayo hayaelezeki na kufikirika, na hisia ambayo ni kuu, ya juu sana kuliko uwezo wa mwanadamu, na inayotamanika, lakini ambayo pia haifikiwi na haipatikani kwa wote.

3 Kazi ya mwili inampatia mwanadamu malengo halisi ya kufuata, maneno halisi, na hisia kwamba Yeye ni halisi na wa kawaida, kwamba ni mnyenyekevu na wa kawaida. Ingawa mwanadamu anaweza kumwogopa, kwa watu wengi Yeye ni rahisi kuhusiana naye: Mwanadamu anaweza kuuona uso Wake, na kuisikia sauti Yake, na hahitaji kumwangalia kwa kutokea mbali. Mwanadamu anahisi kuwa ni rahisi kuufikia mwili huu, sio wa mbali au usioeleweka, bali unaoonekana na kushikika, maana mwili huu upo katika ulimwengu mmoja na mwanadamu. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inahusisha ugumu mwingi usiofikirika, matokeo ambayo yanapatikana mwishowe yanazidi kwa mbali sana kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 175 Ni Mungu Mwenye Mwili Pekee Awezaye Kuwaokoa Binadamu

Inayofuata: 177 Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp