893 Mungu Huwapa Wanadamu Ukweli na Uhai Bure

1 Mungu amewapa wanadamu vitu vya thamani zaidi. Yaani, Mungu aliwapa wanadamu uhai Wake na yote anayo na aliyo bure ili waweze kuishi kwa kuyadhihirisha, ili waweze kubadili yale ambayo Mungu anayo na aliyo na ukweli ambao Yeye huwapa viwe mwelekeo na njia yao ya kuishi, wageuze neno la Mungu kuwa maisha yao, na kutegemea maisha haya kuishi. Pamoja na kuwapa binadamu maisha, hitaji moja Alilo nalo kwao ni kwamba wachukue maisha haya ya Mungu, wayabadilishe kuwa maisha yao wenyewe, na waishi kwa kuyadhihirisha. Mungu anapowaona watu wakiishi kwa kuyadhihirisha maisha haya, Anahisi aliyeridhika.

2 Wakati wanakubali maisha ya Mungu kama maisha yao wenyewe, wanadamu pia wanapata kuelewa ukweli, wanapata kanuni za maana ya kuwa binadamu, wanakuza mizizi wanayohitaji kuwa binadamu, na kupata mwelekeo wanaohitaji kutembea ili kuwa wanadamu. Hawadanganywi na kufungwa na Shetani tena, hawadanganywi na kutumiwa na watu waovu tena, na hawachafuliwi, kutiwa madoa, kufungwa, au kushawishiwa na mienendo mibaya tena. Binadamu wanaishi kwa uhuru kati ya mbingu na dunia, na wameokolewa. Hawajafungwa au kuhisi uchungu tena. Hakuna ugumu tena, wanaishi wakiwa huru na wanaweza kuishi kwa kweli chini ya utawala wa Mungu, wasipitie madhara tena kutokana na nguvu zozote mbaya au za giza. Wanadamu hupata faida kubwa zaidi; wao ndio wanufaishwa wakubwa zaidi.

3 Wakati wanaishi kwa kudhihirisha maisha haya, wakiyachukua maisha haya kama yao wenyewe, hawapitii tena uchungu wowote, lakini badala yake wanaishi kwa furaha na bila ugumu; wanaishi kwa uhuru na wana uhusiano wa kawaida na Mungu. Hawawezi tena kumwasi Mungu au kumpinga; badala yake, wanaweza kuishi kwa kweli chini ya utawala wa Mungu. Wanaishi maisha sahihi na yanayofaa, kutoka ndani hadi nje, na wanakuwa binadamu wa kweli. Ni kwa kukubali tu maisha yanayotoka kwa Mungu ndipo unaweza kuyaokoa maisha yako. Ukiyapata maisha haya, basi maisha yako yatakuwa bila mwisho; huu ni uzima wa milele.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Ndiye Mnufaishwa Mkuu wa Mpango wa Usimamizi wa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 892 Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

Inayofuata: 894 Mungu Huja Kati ya Wanadamu Kuwaokoa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp