272 Mungu Aleta Mwisho wa Binadamu kwa Dunia

1 Maana katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ili kufafanua tabia Yangu ya asili. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—watu hawajapata ufahamu wowote kunihusu kutokana na tabia Yangu. Kwa hivyo, Ninaanza mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, na kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale wanaoniona watajipiga kifuani na kulilia na kuombolezea bila kukoma kwa sababu ya uwepo Wangu.

2 Hii ni kwa sababu Ninaleta mwisho wa wanadamu duniani, na kuanzia sasa na kuendelea, Ninaweka wazi tabia Yangu yote mbele ya wanadamu, ili wote wanijuao na wale wote wasionijua waweze kuyafurahisha macho yao na kuona kwamba kweli, Nimekuja katika ulimwengu wa kibinadamu, Nimekuja duniani ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, na “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Niwaumbe wanadamu. Nawaomba mzingatie kwa makini kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinawakaribia wanadamu tena, kwa wale wote wanaonipinga.

Umetoholewa kutoka katika “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 271 Mungu Huwaokoa Wale Wanaomwabudu Mungu na Kuepuka Uovu

Inayofuata: 273 Uwepo Wa Binadamu Wote Unategemea Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp