963 Mungu Havumilii Kosa Lolote

1 Kuielewa tabia ya haki ya Mungu, kwanza mtu anapaswa kuelewa hisia za Mungu: kile Anachokichukia, kile Anachokichukia kabisa, kile Anachokipenda, ni mvumilivu na mwenye huruma kwa nani, na ni aina gani ya mtu anayepokea rehema hiyo. Hii ni hoja ya msingi kufahamu. Aidha, mtu anapaswa kuelewa kwamba haijalishi Mungu ni mwenye upendo kiasi gani, haijalishi ni Mwenye rehema na upendo kiasi gani kwa watu, Mungu hamvumilii mtu yeyote anayekosea hali na nafasi Yake, wala Hamvumilii mtu yeyote anayekosea heshima Yake. Ingawa Mungu anawapenda watu, Hawadekezi. Anawapatia watu upendo Wake, rehema Yake, na uvumilivu Wake, lakini hajawahi kuwakuwadia; Ana kanuni Zake na mipaka Yake.

2 Bila kujali ni kwa kiwango gani umeuhisi upendo wa Mungu ndani yako, bila kujali upendo huo ni wa kina kiasi gani, hupaswi kamwe kumtendea Mungu kama ambavyo ungemtendea mtu mwingine. Ingawa ni kweli kwamba Mungu anawachukulia watu kama wako karibu Naye, ikiwa mtu anamwangalia Mungu kama mtu mwingine, kana kwamba ni kiumbe mwingine wa uumbaji, kama rafiki au kama kitu cha kuabudu, Mungu atawaficha uso Wake na kuwatelekeza. Hii ndiyo tabia Yake, na watu hawapaswi kulichukulia jambo hili kwa mzaha. Ingawa Mungu anawapenda watu, Hawadekezi. Anawapatia watu upendo Wake, rehema Yake, na uvumilivu Wake, lakini hajawahi kuwakuwadia; Ana kanuni Zake na mipaka Yake.

3 Mara nyingi sisi huona maneno kama haya yakinenwa na Mungu kuhusu tabia Yake: Haijalishi umesafiri njia nyingi kiasi gani, umefanya kazi kubwa kiasi gani au umevumilia kiasi gani, mara tu unapoikosea tabia ya Mungu, Atamlipa kila mmoja wenu kulingana na kile ulichokifanya. Watu wanapomkosea Mungu, inaweza isiwe kwa tukio moja, au kitu kimoja walichokisema, bali ni kwa sababu ya mtazamo walionao na hali waliyomo. Hili ni jambo la kutisha sana. Hivyo, hupaswi kusahau kwamba haijalishi ni kwa namna gani Mungu anawachukulia watu, haijalishi ni namna gani Anafikiri juu ya watu, nafasi, tabia na hadhi ya Mungu kamwe havibadiliki. Kwa binadamu, Mungu siku zote ni Bwana wa vitu vyote na Muumbaji.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 962 Tabia ya Mungu Yenye Haki Haistahimili Kosa Lolote

Inayofuata: 964 Kila Kitu Afanyacho Mungu ni cha Haki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp