639 Umuhimu Mkubwa wa Mungu Kuwachagua Watu Hawa
1 Kama mtu binafsi katika mkondo huu, kila mtu anapaswa kujua lengo la mpango mzima wa usimamizi wa Mungu ni nini, ukweli ambao Mungu tayari ametimiza, kwa nini Mungu amelichagua kundi hili la watu, malengo yake na umuhimu wake ni upi, na kile ambacho Mungu anataka kufanikisha katika kundi hili. Katika nchi ya joka kuu jekundu, Mungu ameweza kuinua kundi kama hilo la watu wasioonekana kwa urahisi, na Ameendelea kufanya kazi hadi sasa, Akijaribu na kuwakamilisha kwa kila namna, Akizungumza maneno yasiyohesabika, Akifanya kazi kubwa na kutuma vitu vingi vya kuhudumu. Kutokana na Mungu kukamilisha kazi kubwa kiasi hicho, inaweza kuonekana kwamba umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa sana. Bado hamuwezi kuielewa kabisa.
2 Kwa hiyo, msiichukulie kazi ambayo Mungu amefanya kwenu kama suala dogo; hiki si kitu kidogo. Kile tu ambacho Mungu amewaonyesha leo kinawatosha kutafakari na kukielewa. Mkielewa tu kwa kweli na kwa kina ndipo mtaweza kupata uzoefu wa kina zaidi na kupiga hatua katika maisha yenu. Kile ambacho watu wanakielewa na kukifanya sasa ni kidogo sana na hakiwezi kukidhi kikamilifu makusudi ya Mungu. Huu ndio upungufu wa wanadamu na kushindwa kutimiza wajibu wao. Hii ndiyo maana matokeo ambayo yangepaswa kufikiwa bado hayajafikiwa.
Umetoholewa kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili