69 Umuhimu wa Kazi ya Ushindi

1 Kazi ya ushindi inafanikisha mazao yake kwa kuchukua hatima na matarajio ya mwanadamu na kuhukumu na kuadibu uasi wa tabia ya mwanadamu. Haifanikishwi kwa kufanya mpango na mwanadamu, yaani, kwa kumpa mwanadamu baraka na neema, lakini ni kwa kufichua uaminifu wa mwanadamu kwa kumnyang’anya “uhuru” wake na kukomesha matarajio yake. Hiki ni kiini cha kazi ya ushindi. Tatizo kubwa mno kwa mwanadamu ni kuwa yeye hufikiria tu kuhusu hatima yake na matarajio, na kuyaabudu. Mwanadamu humfuata Mungu kwa ajili ya hatima yake na matarajio; yeye hamwabudu Mungu kwa sababu ya upendo wake kwake. Na kwa hivyo, katika ushindi kwa mwanadamu, ubinafsi wa mwanadamu, uroho na vitu ambavyo sana sana huzuia ibada yake kwa Mungu ni sharti vishughulikiwe na hapo viondolewe. Kwa kufanya hivyo, matokeo ya ushindi kwa mwanadamu yatatimizwa.

2 Katika ushindi wa kwanza wa mwanadamu ni muhimu kuondoa matarajio makubwa na udhaifu mkubwa kabisa wa mwanadamu, na, kupitia hili, kufichua upendo wa mwanadamu kwa Mungu, na kubadilisha maarifa yake kuhusu maisha ya binadamu, mtazamo wake kwa Mungu, na maana ya kuwepo kwake. Kwa njia hii, upendo wa mwanadamu kwa Mungu unatakaswa, ambapo ni kusema, moyo wa binadamu unashindwa. Lakini katika mtazamo wake wa viumbe vyote, Mungu hashindi kwa sababu ya kushinda; badala yake, Yeye anashinda ili kumpata mtu, kwa sababu ya utukufu wake mwenyewe, na ili kuokoa ufanano wa kwanza wa awali wa mwanadamu. Ni upato wa mwanadamu tu kufuatia ushindi wake na ujio wake wa mwisho katika hatima ya ajabu ndiyo yaliyomo katika kiini cha kazi yote ya wokovu, na ni hii tu ndio inayoweza kufikia lengo la wokovu wa mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 68 Lengo Kuu la Kazi ya Mungu ya Ushindi

Inayofuata: 70 Watu Waaninishwa na Kazi ya Ushindi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp