53 Mungu Atawashinda Watu wa Mataifa Yote

1 Wakati wa uumbaji, Nilikuwa tayari Nimeamua kwamba kazi Yangu duniani itakamilika katika enzi ya mwisho. Wakati ambapo kazi Yangu itaisha ndio hasa wakati ambapo mambo Yangu yote yatadhihirishwa katika anga. Nitawafanya watu walio duniani wakubali mambo Yangu, na mbele ya “kiti cha hukumu,” matendo Yangu yatathibitishwa, ili yakubalike miongoni mwa watu walio kote duniani, ambao watasalimu amri. Hivyo, baadaye, Nitaanzisha shughuli ambayo haijawahi kamwe kutekelezwa katika enzi zilizopita. Tangu leo na kuendelea, Nitatoa waziwazi matendo Yangu hatua kwa hatua, ili hekima Yangu, ajabu Yangu, na kutoeleweka Kwangu vitakubaliwa na kuthibitishwa katika kila eneo la jamii.

2 Tangu wakati huu na kuendelea, matendo Yangu yatatambuliwa na kila eneo la jamii, na huu utakuwa wakati ambapo Nitapata utukufu wote duniani. Katika wakati huo, Nitamwonekania mwanadamu na Sitajificha tena. Wakati huu, matendo Yangu bado hayajafika kilele. Kazi Yangu inaendelea mbele, na wakati ambapo itafika kilele chake ndio wakati ambapo itamalizika. Nitawashinda kabisa watu wa mataifa yote, Nitasababisha wanyama wakali wageuke kuwa wa kuweza kufugwa kama wanakondoo mbele Yangu, na Nitasababisha joka kubwa jekundu kutii mbele Yangu kama watu walio duniani. Nitawashinda adui zangu wote mbinguni, na Nitasababisha washindani Wangu wote duniani kushindwa. Huu ni mpango Wangu, na ajabu ya matendo Yangu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 42” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 52 Msifu Mungu Ambaye Amerudi Akiwa Mshindi

Inayofuata: 54 Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp