288 Mungu Atasahihisha Udhalimu wa Dunia ya Binadamu

1 Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakataza maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui Wangu wote waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni, hasira imechanganywa, Nitaukanyaga ulimwengu wote sawasawa, bila kumwacha yeyote, na kuwatia maadui Wangu hofu kubwa. Naiangamiza dunia nzima, na kuwafanya maadui Wangu waanguke katika maangamizo hayo, ili kuanzia sasa na kuendelea wasiwapotoshe wanadamu tena.

2 Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeubadilisha. Ninapotembeatembea kwa fahari kuu ulimwenguni, wanadamu wote watafanywa wapya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwanadamu hatalia tena, hatanililia tena akitaka msaada. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo … Leo hii, miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, Ninaendeleza kazi Niliyokusudia kukamilisha. Ninamtembelea kila mmoja, Nikifanya kazi Yangu jinsi Nilivyopanga, na binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine kulingana na mapenzi Yangu.

3 Watu walio duniani wameweka mawazo yao kwa hatima zao wenyewe, kwa maana siku yenyewe hakika inakaribia na malaika wanacheza parapanda zao. Hakutakuwa na kuchelewa tena, na kila kiumbe ataanza kucheza kwa shangwe. Ni nani anayeweza kusongeza siku Yangu kwa uwezo wake? Inawezekana kiwe kiumbe cha duniani? Zinaweza kuwa nyota angani au malaika? Ninapotoa tamko la kuanza ukombozi wa wana wa Israeli, siku Yangu inawaelekea watu wote wa ulimwengu. Kila mwanadamu anahofia kurejea kwa taifa la Israeli. Israeli itakaporejea, hiyo itakuwa siku Yangu ya utukufu, na pia, itakuwa siku ambayo kila kitu kitabadilika na kuwa kipya.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 27” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 287 Mwanadamu Anadhibiti Majaliwa Yake Mwenyewe?

Inayofuata: 289 Mungu Apitia Shida za Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp