1011 Mungu Aamua Mwisho wa Watu Kulingana na Asili Yao

1 Kama mtu anaweza kusalimika hatimaye, ni kwa sababu amefikia mahitaji ya Mungu, na kama mtu hawezi hatimaye kubaki katika kipindi cha pumziko, ni kwa sababu mtu huyu hamtii Mungu na hajakidhi mahitaji ya Mungu. Kila mtu ana hatima inayofaa. Hatima hizi zinaamuliwa kulingana na asili ya kila mtu na hazihusiani kabisa.

2 Mwenendo ovu wa mtoto hauwezi kuhamishwa kwa wazazi wake, na haki ya mtoto haiwezi kushirikishwa wazazi wake. Mwenendo ovu wa mzazi huwezi kuhamishwa kwa watoto wake, na haki ya mzazi haiwezi kushirikishwa watoto wake. Kila mtu anabeba dhambi zake husika, na kila mtu anafurahia bahati yake husika. Hakuna anayeweza kuchukua ya mwingine. Hii ni haki. Hakuna awezaye kubeba dhambi za mwingine; hata zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kupokea adhabu badala ya mwingine. Hii ni thabiti.

3 Wanaotenda haki ni wanaotenda haki, na watenda maovu ni watenda maovu. Watenda haki watasalimika, na watenda maovu wataangamizwa. Watakatifu ni watakatifu; wao si wachafu. Wachafu ni wachafu, na hawana sehemu yoyote takatifu. Watu wote waovu wataangamizwa, na watu wote wa haki watasalimika, hata kama watoto wa watenda maovu wanafanya matendo ya haki, na hata kama wazazi wa mtu wa haki wanafanya matendo maovu.

4 Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisizolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia. Wanaofanya wajibu wao na wasiofanya ni adui, wanaompenda Mungu na wanaomchukia Mungu ni wapinzani. Wanaoingia rahani na wale ambao wameangamizwa ni aina mbili ya viumbe wasiolingana.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1010 Mipangilio ya Mungu ya Matokeo ya Watu Wote

Inayofuata: 1012 Wanaoamini na Wasioamini Hawalingani Kabisa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp