530 Anachochukia Mungu Zaidi ni Ukaidi na Uhalifu wa Mwanadamu

1 Hali ya mwanadamu haibadiliki kamwe. Kilicho ndani ya mioyo yao sio kulingana na mapenzi Yangu—sio Ninachohitaji. Jambo Ninalochukia zaidi ni ugumu na uhalifu sugu wa mwanadamu na ukaidi sugu, lakini ni nguvu zipi ambazo huwachochea wanadamu waendelee kushindwa kunijua, kuwafanya waniweke mbali na wao kila mara, na kutotenda kulingana na mapenzi Yangu mbele Yangu kamwe lakini kunipinga nyuma Yangu? Je, huu ndio uaminifu wao? Huu ndio upendo wao Kwangu? Mbona wasitubu dhambi zao na kuzaliwa mara ya pili? Mbona binadamu hupenda kuishi kwenye chemichemi badala ya kuishi mahali pasipo na matope? Inawezekana kuwa Mimi Nimewadhulumu? Inawezekana kuwa Mimi Nimewapotosha? Inawezekana kuwa Mimi nimewaelekeza kuzimu?

2 Kila mtu anataka kuishi “kuzimu.” Mwangaza unapotokea, macho yao hupofuka ghafla, kwa kuwa kila chao kinatoka kuzimu. Ilhali watu hawana ufahamu wa mambo haya na wanafurahia tu “raha za motoni.” Wao hata hushikilia kwa nguvu karibu na vifua vyao kama hazina wakihofu kwamba Mimi nitazinyakua hazina hizi, hivyo kuwaacha bila kiini cha kuwepo kwao. Wanadamu wananiogopa na ndio maana wao hukaa mbali na Mimi na kutokaa karibu Nami Ninapokuja duniani kwa maana “hawapendi kujiletea madhara,” wakiwa na ombi la kuishi maisha ya amani katika familia yao ili wawe na “maisha ya furaha duniani.”

3 Kunzia wakati Nifikapo, amani inatoweka katika nyumba zao. Nakusudia kusambaratisha mataifa yote yatawanyike, sembuse familia ya mwanadamu. Ni nani awezaye kuepuka mkono Wangu? Itawezekanaje kuwa wale wanaopokea baraka wataepuka kwa sababu ya kutonuia kwao? Itawezekanaje kamwe kuwa wale walioadibiwa watapata huruma Yangu kwa sababu ya wao kuwa na woga? Katika maneno Yangu yote, wanadamu wameona mapenzi Yangu na kuona matendo Yangu, lakini ni nani awezaye kuondokana na minyororo ya mawazo yake mwenyewe? Ni nani anaweza kupata njia kutoka ndani au nje ya maneno Yangu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 27” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 529 Usijifurahishe kwa Sababu Mungu ni Mvumilivu

Inayofuata: 531 Mwanadamu ni Mgumu Sana Kuokoa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp