1013 Mungu Hawaokoi Waovu
Kwa maana wengi waovu wameingia ndani kimya wakati Niko kazini, lakini Sina haraka ya kuwafukuza. Badala yake, Nitawatawanya wakati utakapofika. Ni baada ya hapo tu ndipo Nitakuwa chemchemi ya uzima, kuwakubalia wanaonipenda kweli wapokee kutoka Kwangu tunda la mtini na harufu ya yungiyungi. Katika nchi ambako Shetani huishi, nchi ya vumbi, hakuna dhahabu safi iliyobaki, ila ni mchanga tu, na kwa hiyo, Nikikabiliwa na hali hizi, Nafanya hatua hiyo ya kazi. Lazima ujue kwamba Ninachopata ni dhahabu safi, iliyosafishwa, wala si mchanga. Ni jinsi gani waovu wanaweza kubaki katika nyumba Yangu? Ninawezaje kuruhusu Mbweha kuwa vimelea ndani ya paradiso Yangu? Natumia kila mbinu inayoweza kufikiriwa kuvifukuza vitu hivi. Kabla ya mapenzi Yangu kufichuliwa, hakuna anayefahamu Ninachotaka kufanya. Nikichukua fursa hii, Ninawafukuza wale waovu, na wanalazimika kuondoka machoni Pangu. Hili ndilo Mimi huwafanyia waovu, lakini bado kutakuwa na siku ya wao kunifanyia huduma.
Umetoholewa kutoka katika “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni” katika Neno Laonekana katika Mwili