825 Mungu Amsihi Mwanadamu Amshuhudie Tu

1 Hiyo ndiyo maana Nina wasiwasi kwa sababu yenu: Akiachwa kuishi maisha peke yake, je, mwanadamu atapata kuwa bora ikilinganishwa na hali ilivyo sasa? Je, hamna wasiwasi kuhusu hali zenu za kitoto? Mnaweza hakika kuwa kama watu wateule wa Uyahudi, kuwa waaminifu Kwangu pekee Yangu katika kila hali? Kile mnachodhihirisha sio mchezo wa watoto ambao wametangatanga kutoka wazazi wao, bali ni unyama unaoonekana katika wanyama ambao wako mbali na mjeledi wa mchungaji wao. Mnapaswa kujua hali yenu halisi, ambayo pia ni udhaifu mlio nao nyote, ambao ni ugonjwa mlio nao nyote. Kwa hivyo ombi Langu la pekee kwenu ni kwamba muwe na ushahidi Kwangu. Msije katika hali yoyote kuyaruhusu maradhi ya zamani kuchipuka tena. Jambo la muhimu zaidi ni kutoa ushuhuda. Hicho ndicho kiini cha kazi Yangu. Mnafaa kuyakubali maneno Yangu jinsi Maria alivyokubali ufunuo wa Yehova uliomjia kupitia kwenye ndoto, kuamini na kisha kutii. Hili pekee ndilo linakubalika kama kuwa mtakatifu.

2 Kwa maana ni ninyi ndio mnasikia neno Langu zaidi, na ambao wamebarikiwa zaidi na Mimi. Ninawapa mali Yangu yote ya thamani, kuwakabidhi kila Nilicho nacho. Hali yenu na ile ya Wayahudi, hata hivyo, ni tofauti kabisa, ni kama nchi mbili tofauti. Lakini mkilinganishwa nao, mnapokea baraka nyingi zaidi yao. Huku wao wakisubiri kwa hamu ili kujitokeza Kwangu, muda mwingi Nimekuwa na ninyi, kutumia utajiri Wangu kwa pamoja. Kwa ulinganisho, ni nini kinachowapa haki ya kunifokea na kuzozana na Mimi na kudai sehemu za mali Yangu? Hampati vya kutosha? Ninawapa vingi sana, lakini Mnachonipa ni huzuni wa kuvunja moyo na dhiki na chuki isiyokomeshwa na kutoridhika. Mnakuwa wazushi sana, ilhali bado mnaiamsha huruma Yangu. Kwa hivyo sina la kufanya ila kuizima chuki Yangu yote na kunena kupinga Kwangu kwenu tena na tena.

Umetoholewa kutoka katika “Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 824 Akili Anayopaswa Kuwa Nayo Mwanadamu Baada ya Kushindwa

Inayofuata: 826 Wajibu Wako kama Muumini ni Kumshuhudia Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp