876 Mungu Kupitia Maumivu ya Mwanadamu ni kwa Maana Sana

1 Kupata mwili kukifanya kazi katika hatua hizi mbili kwa njia hii inamaanisha kuwa zimefanywa vizuri kabisa na kuwa zimetengeneza mlolongo. Kwa nini Ninasema zimetengeneza mlolongo? Ni kwa sababu kazi ambayo imefanywa katika hatua hizi mbili na kupata mwili kwa kwanza na kupata mwili kwa sasa inatatua mateso yote katika maisha ya mwanadamu na uchungu wa mwanadamu mwenyewe. Uchungu wa kuzaliwa, kufa, magonjwa na uzee uliopo katika maisha yote ya mwanadamu ulitoka wapi? Je, mwanadamu alikuwa na vitu hivi alipoumbwa mara ya kwanza? Hakuwa navyo, sivyo? Vitu hivi vilikuja baada ya wanadamu kujaribiwa na Shetani na miili yao ikasawijika. Uchungu wa mwili, mateso yake na utupu wake, na pia masuala yenye taabu sana ya dunia ya binadamu yote yalikuja baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, kutoka wakati Shetani alipoanza kuwatesa watu. Hivyo ili kuleta hatima ya ajabu unaomngoja mwanadamu mbali na mfumbato wa Shetani, Mungu lazima apitie mateso haya Mwenyewe.

2 Wakati huo, kupata mwili uliokuwa Yesu uliiondoa sheria, ukaitimiza sheria na kuileta Enzi ya Neema. Alileta huruma na upendo kwa mwanadamu na kisha akasulubiwa, hivyo kusamehe dhambi zote za mwanadamu. Kwa kulipa gharama, mwanadamu angerejeshwa. Baada ya mwanadamu kukombolewa, alisamehewa dhambi zake. Bado yeye ni mwenye dhambi. Mwanadamu amepotoshwa na Shetani na hivyo bado ni mwenye dhambi, na huu ni ukweli. Bado kuna mambo fulani ya kimawazo ndani ya binadamu au roho ambayo yanaweza kudhibitiwa na kutawaliwa na Shetani. Hii ndiyo maana haiwezekani kwako kuwa na magonjwa, matatizo na kuhisi mwenye kutaka kujitia kitanzi na wakati mwingine pia kuhisi huzuni ya dunia, au kwamba maisha hayana maana. Hiyo ni kusema, kuteseka huku bado kuko chini ya uongozi wa Shetani; ni mojawapo ya udhaifu wa kusababisha mauti wa mwanadamu.

3 Shetani bado ana uwezo wa kutumia vile vitu ambavyo amevipotosha na kuvikanyagia chini—ni silaha ambazo Shetani anaweza kutumia dhidi ya mwanadamu. Kufuatia hilo, Mungu mwenye mwili alianza hatua ya pili ya kazi, Akiumia kwa niaba ya mwanadamu kwa wakati uo huo Akifanya kazi ya ushindi. Kwa kupata mwili kulipa gharama ya mateso, udhaifu wa kusababisha mauti katika mwanadamu utafikishwa kikomo na kusuluhishwa. Baada ya kupitia kwa uchungu duniani kumrejesha mwanadamu, Shetani hatakuwa na mshiko tena kwa mwanadamu na mwanadamu atamgeukia Mungu kikamilifu. Hili tu ndilo linaloweza kuitwa binadamu kumilikiwa na Mungu kikamilifu. Kupitia uchungu wa dunia kwa kupata mwili na kustahimili Kwakeuchungu huu kwa niaba ya binadamu si jambo lisilo la maana. Ni jambo la muhimu sana.

Umetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Mungu Kuuonja Mateso ya Dunia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 875 Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu ili Ateseke kwa Niaba ya Mwanadamu

Inayofuata: 877 Mungu Huvumilia Aibu Kubwa Kuwaokoa Wanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp