693 Mungu Hatimaye Huwapata wale Walio na Ukweli

1 Watu ambao wamezaliwa siku za mwisho ni watu wa aina gani? Ni wale ambao wamepitia miaka mingi ya upotovu wa Shetani, ambao wamepotoshwa kwa kina sana kiasi kwamba hawana mfanano wa binadamu tena. Lakini hatimaye, baada ya kupitia hukumu, kuadibu na kufunuliwa kwa neno la Mungu, baada ya kushindwa, wanapata ukweli kutoka ndani ya maneno ya Mungu na wanashawishiwa kwa dhati na Mungu; wanafikia uelewa wa Mungu na wanaweza kutii Mungu kikamilifu na kuyakidhi mapenzi Yake. Mwishowe, kundi la watu wanaopatwa kupitia mpango wa Mungu wa usimamizi watakuwa watu kama hawa. Watu watakaopatwa katika mpango mzima wa usimamizi ni kundi linaloweza kuelewa mapenzi ya Mungu, wanaoupata ukweli kutoka kwa Mungu, na wanaomiliki aina ya maisha na mfanano wa binadamu ambao Mungu anahitaji.

2 Mwanadamu alipoumbwa kwanza, alionekana tu kama binadamu na alikuwa na uhai. Lakini hakufanana na binadamu ndani yake ambako Mungu alihitaji ama alimtumania kufikia. Kundi la watu ambao watapatwa mwishowe ni wale ambao watabaki mwishowe, na pia ni wale ambao Mungu anawahitaji, ambao Amefurahishwa nao na ambao wanamridhisha. Katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu kadhaa, hawa watu wamepata zaidi, ambayo yametokana na kunyunyiziwa na Mungu na yamepewa mwanadamu kwa njia ya vita Vyake na Shetani. Watu katika kundi hili ni bora kuliko wale ambao Mungu aliwaumba mwanzoni kabisa; hata ingawa wamepitia upotovu, hili haliwezi kuepukika, na ni suala ambalo liko katika wigo wa mpango wa Mungu wa usimamizi ambao unafichua uweza Wake na hekima Yake vya kutosha na zaidi, ukifichua pia kwamba yote ambayo Mungu amepanga, kunuia na kutimiza ni kubwa zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kuujua Uweza wa Mungu Pekee Ndipo Unaweza Kuwa na Imani ya Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 692 Mtazamo Wa Mwanadamu Kwa Majaribu

Inayofuata: 694 Ufahamu wa Petro Kuhusu Kuadibu na Hukumu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp