972 Mungu Huongoza Maisha ya Mwanadamu Daima
1 Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo daima Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, si kila kitu anachofanya Mungu ni cha kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu kuishi maisha ya kawaida? Iwe ili mwanadamu ashike kanuni Zake ama ashike sheria Zake, lengo la Mungu ni kwa mwanadamu kutomwabudu Shetani, kutodhuriwa na Shetani; hili ndilo la msingi zaidi, na hili ndilo lililofanywa mwanzoni kabisa. Ingawa Ana mipango na nia kwa mwanadamu, Hajifanyii chochote. Kila kitu Anachofanya kinafanyiwa mwanadamu tu, kumlinda mwanadamu, kumhifadhi mwanadamu dhidi ya kupotezwa.
2 Wakati huelewi ukweli, Mungu hukuongoza vipi? Anaangaza mwangaza kwako, akikwambia wazi kwamba haya hayaambatani na ukweli, na kile unachofaa kufanya. Wakati Mungu anakuongoza, Anapokukimu, Anapokusaidia na kukufadhili, unahisi urafiki wa Mungu, kuheshimika Kwake, unahisi jinsi Anavyopendeza, jinsi Alivyo mwema. Lakini Mungu anaposhutumu upotovu wako, ama Anapokuhukumu na kukufundisha nidhamu kwa sababu ya kuasi dhidi Yake, anakushutumu kwa kutumia maneno? Anakufundisha nidhamu kupitia mazingira yako na kupitia kwa watu, masuala na mambo? Mungu anafanya kazi kwa njia ya upole, laini, yenye upendo na ya kujali, kwa njia iliyopimwa kwa namna ya ajabu na sahihi. Njia Yake haikufanyi uhisi hisia kali ya mhemuko kama vile. Mungu kamwe hakupi mawazo makali ya aina hiyo ama hisia kali zinazofanya mambo kutovumilika.
3 Mungu hutumia maneno Yake, ukweli Wake na uhai Wake kuendelea bila kusita kumkimu mwanadamu, kumfadhili mwanadamu. Upendo Wake kwa mwanadamu, kuthamini na utunzaji Wake wa mwanadamu haviwezi kuelezwa wazi kwa sentensi moja au mbili. Si kitu kinacholetwa na kujisifu kwa mwanadamu lakini ni kitu ambacho Mungu analeta kupitia kwa vitendo halisi; ni ufunuo wa kiini cha Mungu. Yote ambayo Mungu anampa mwanadamu, yakiwemo maneno ya Mungu, njia tofauti ambazo kwazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu, kile ambacho Mungu anamwambia mwanadamu, kile ambacho Mungu anamkumbusha mwanadamu kuhusu, kile ambacho Anashauri na kutia moyo, vyote vimetoka kwa kiini kimoja: Vyote vimetoka kwa utakatifu wa Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV” katika Neno Laonekana katika Mwili