12 Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki

Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauchukua na baadaye Nikawaleta Waisraeli Mashariki, na vilevile binadamu wote Mashariki. Nimewaleta wote kwenye nuru ili waweze kuungana tena nayo, na kushirikiana na nuru, na wasilazimike kuitafuta tena. Nitawaacha wote wanaotafuta waione nuru tena na kuuona utukufu Niliokuwa nao katika Israeli; Nitawaacha waone kwamba tayari Nimeshuka juu ya wingu jeupe miongoni mwa wanadamu, kuwaacha waone mawingu mengi meupe na vishada vingi vya matunda, na, zaidi ya hayo, Nitawaacha wamwone Yehova Mungu wa Israeli. Nitawaacha waone Mkuu wa Wayahudi, Masihi aliyengojewa kwa hamu, na kuonekana kamili kwa Mimi niliyeteswa na wafalme kotekote katika enzi. Nitafanya kazi katika ulimwengu mzima na Nitatekeleza kazi kubwa, Nikifichua utukufu Wangu wote na matendo Yangu yote kwa mwanadamu katika siku za mwisho. Nitaonyesha uso Wangu uliojaa utukufu kwa wale ambao wameningoja kwa miaka mingi, kwa wale ambao wametamani kuniona Nikija juu ya wingu jeupe, kwa Israeli ambayo imengoja Nionekane kwa mara nyingine, na kwa wanadamu wote wanaonitesa, ili wote wajue kwamba Niliuchukua utukufu Wangu zamani na kuuleta Mashariki, Ili usiwe katika Uyahudi tena. Kwani siku za mwisho tayari zimewadia!

Umetoholewa kutoka katika “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 11 Tumenyakuliwa Hadi Mbele ya Kiti cha Enzi

Inayofuata: 13 Utukufu wa Mungu Wang’aa Kutoka Mashariki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp