33 Mungu Amefanya Kazi Mpya Katika Ulimwengu Mzima

1 Nitajaza mbingu na maonyesho ya kazi Yangu, ili kila kitu kilicho chini ya ardhi kisujudu chini ya nguvu Zangu, Nikitekeleza mpango Wangu wa “umoja wa ulimwengu” na kusababisha hili tamanio Langu moja kufaulu, na ili binadamu wasiweze “kuzurura kote” juu ya uso wa dunia lakini wapate hatima ya kufaa bila kuchelewa. Naifikiria jamii ya binadamu kwa kila njia, Nikifanya hilo ili kwamba wanadamu wote waje kuishi katika nchi ya amani na furaha hivi punde, ili siku za maisha yao zisiwe na huzuni na ukiwa tena, na ili mpango Wangu hautakuwa bure duniani.

2 Kwa kuwa mwanadamu yupo pale, Nitalijenga taifa Langu duniani, kwani sehemu ya maonyesho ya utukufu Wangu iko duniani. Juu mbinguni, Nitaiweka miji Yangu kwenye haki na hivyo kufanya kila kitu kiwe kipya juu na chini. Nitaleta yote yaliyopo juu na chini ya mbingu kuwa katika umoja, ili vitu vyote duniani viungane na vyote vilivyo mbinguni. Huu ndio mpango Wangu, ndio Nitakaoutimiza katika enzi ya mwisho—mtu asiingilie^ sehemu hii ya kazi Yangu!

3 Nitawafanya wanadamu ulimwenguni kote kutii mbele ya kiti Changu cha enzi, Nikiwagawanya katika makundi mbalimbali kulingana na hukumu Yangu, Nikiwaainisha kulingana na makundi haya, na kuwaainisha zaidi katika jamii zao, ili binadamu wote wakome kuniasi, badala yake waingie katika mpango mzuri na wa taratibu kulingana na makundi ambayo Nimeyataja—mtu yeyote asitembee huku na huko bila kufikiria! Katika ulimwengu wote, Nimefanya kazi mpya; katika ulimwengu wote, binadamu wote hutunduwaa na kupigwa na bumbuwazi kwa kuonekana Kwangu kwa ghafla, upeo wao wa macho ulibubujika kwa namna ambayo haijawahi kutendeka awali kwa ajili ya kuonekana Kwangu wazi. Je, leo haiko hivi hasa?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 43” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 32 Mungu Atarudisha Hali ya Kitambo ya Uumbaji

Inayofuata: 34 Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki