957 Mungu Atumai Mwanadamu Atubu kwa Kweli

1 Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo ya gunia pamoja na jivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwao kwa dhambi zao—Mungu alikuwa angali na ghadhabu na wao. Baada ya wao kupitia mfululizo wa vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ikabadilika kwa utaratibu kuwa huruma na uvumilivu kwao.

2 Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu wa vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika tukio lilo hilo. Mungu alionyesha na kufichua viini hivi viwili tofauti kabisa kwa mfululizo wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na kutokosewa kwa kiini cha Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu havumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli mara nadra kwa Mungu, na ni nadra kwa watu kugeuka kwa kweli kutoka kwa njia zao ovu na kuacha vurugu iliyo mikononi mwao.

3 Wakati Mungu ameghadhabishwa na binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kumpa binadamu huruma na uvumilivu Wake kwa ukarimu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo mbovu wa mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu kwa kweli mbele Yake, kwa wale wanaoweza kugeuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha vurugu iliyo mikononi mwao. Mtazamo wa Mungu ulifichuliwa waziwazi sana katika jinsi Alivyowatendea Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu si vigumu kuvipokea hata kidogo; Anahitaji toba ya kweli ya mtu. Mradi tu watu wageuka kutoka kwa njia zao ovu na kuuacha vurugu iliyo mikononi mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 956 Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu

Inayofuata: 958 Kanuni za Mungu za Kutenda Hazibadiliki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp