868 Mungu Katika Mwili Hufanya Kazi Kimya ili Kuwaokoa Wanadamu

1 Na bado ni huyu mtu wa kawaida, aliyefichika kati ya watu, ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hatupi maelezo yoyote, wala Hatuambii kwa nini amerudi, lakini Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua zilizopimwa, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole na laini mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—lakini hakuna inayompa mwanadamu huruma na kumtia hofu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa tumejaa aibu isiyovumilika, tusijue pa kujificha.

2 Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kupitia Kwake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Lakini tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Bado, kama awali Yeye kwa unyenyekevu, hufanya kazi Yake akiwa amefichwa ndani ya mwili, akipeana maonyesho a moyo Wake wa ndani zaidi, kana kwamba hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, kana kwamba yeye milele husamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele huvumilia mtazamo wa mwanadamu Kwake usioheshimu.

3 Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa.

Umetoholewa kutoka katika “Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 867 Mungu ni Msaada wa Milele wa Mwanadamu

Inayofuata: 869 Mungu Ateseka Sana Kumwokoa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp