175 Ni Mungu Mwenye Mwili Pekee Awezaye Kuwaokoa Binadamu

1 Sababu pekee ambayo Mungu mwenye mwili amefanyika mwili ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu aliyepotoka. Kwa wale wanaotaka kuokolewa, thamani ya Roho ipo chini zaidi kulinganisha na ile ya mwili. Kazi ya Roho inaweza kuufikia ulimwengu wote, katika milima yote, mito, maziwa, na bahari, lakini kazi ya mwili kwa ufanisi zaidi inahusiana na kila mtu anayekutana na Yeye. Aidha, mwili wa Mungu katika umbo la kushikika unaweza kueleweka vizuri na kuaminiwa na mwanadamu, na unaweza kuimarisha maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na anaweza kumwachia mwanadamu mvuto wa kina wa matendo halisi ya Mungu.

2 Kazi ya Roho imefungwa sirini, ni vigumu kwa viumbe wenye mwili wa kufa kuelewa, na vigumu zaidi kwao kuona, na hivyo wanaweza kutegemea tu vitu vya kufikirika. Hata hivyo, kazi ya mwili ni ya kawaida, na imejikita katika uhalisi, na ina hekima kubwa sana, na ni ukweli unaoweza kuonekana kwa macho ya mwanadamu; mwanadamu anaweza kupitia uzoefu wa hekima ya Mungu, na hana haja ya kuwa na fikira zake kubwa. Huu ndio usahihi na thamani halisi ya kazi ya Mungu mwenye mwili.

3 Roho anaweza tu kufanya vitu ambavyo havionekani kwa mwanadamu na vigumu kwake kufikiria, hivi havitoi maana inayoeleweka. Vinatoa maana ya kusonga, au ya jumla tu, na havitoi maelekezo kwa maneno. Hata hivyo, kazi ya Mungu mwenye mwili, ni tofauti sana: Ina mwongozo sahihi wa maneno, ina nia ya wazi, ina malengo ya wazi yanayohitajika.

4 Kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi yenye kuwezekana tu, na uongozi wa wakati ndio unaofaa kwa ladha ya mwanadamu, na kazi halisi ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika tabia yake iliyopotoka na kusawijika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake ndiye Anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 174 Mungu Mwenye Mwili Pekee Ndiye Awezaye Kumwokoa Mwanadamu Kikamilifu

Inayofuata: 176 Mungu Alikuwa Mwili Kufanya Kazi kwa Ajili ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp