202 Mungu Mwenye Mwili Ni wa Maana Sana Kwako
1 Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako?
2 Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu?
3 Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu.
Umetoholewa kutoka katika “Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili