112 Mungu Ni Mwanzo na Mwisho
Mimi ndiye Mwanzo na Mwisho: Mimi ndiye Mpanzi na Mvunaji.
1 Nyote mnafahamu kuwa Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho; ni Yeye Mwenyewe ndiye Anayeanzisha kazi Yake na hivyo lazima iwe ni Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani na huishinda dunia. Kila wakati Yeye Mwenyewe Anapofanya kazi miongoni mwa mwanadamu, ni mwanzo wa mapigano mapya. Bila mwanzo wa kazi mpya, kwa kawaida hakutakuwa na kikomo kwa enzi ya kale. Na bila kikomo kwa enzi ya kale ina maana kuwa vita na Shetani havijafika mwisho.
2 Ni kama tu Mungu Mwenyewe Anakuja miongoni mwa mwanadamu na kutenda kazi mpya ndipo mwanadamu atakapoweza kujitoa kutoka katika umiliki wa Shetani na kupata maisha na mwanzo mpya. Vinginevyo, mwanadamu ataishi milele katika wakati wa kale na milele kuishi katika ushawishi wa kale wa Shetani. Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale ambao humfuata Yeye.
Mimi ndiye Mwanzo na Mwisho: Mimi ndiye Mpanzi na Mvunaji.
Umetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili