865 Mungu Asikitishwa na Uovu na Upotovu wa Wanadamu
1 Wakati Mungu anapokuwa mwili, kugeuka ndani wa wastani, mtu wa kawaida akiishi miongoni mwa wanadamu, miongoni mwa watu. Mbinu, sheria, n.k za kuishi kwa wanadamu,—zote hizi zimeundwa kwa misingi ya mantiki, maarifa na falsafa ya Shetani. Wanadamu wanaoishi chini ya aina hizi za sheria hawana ubinadamu, hawana ukweli—wote wanaukataa ukweli, na ni wakatili kwa Mungu. Tunaona kwamba kiini Chake ni kinyume kabisa na mantiki, maarifa na falsafa ya Shetani. Kiini Chake kimejaa haki, ukweli, na utakatifu na uhalisi mwingine wa mambo yote mazuri. Mungu, akimiliki kiini hiki na Akiishi miongoni mwa wanadamu—Anahisi vipi katika moyo Wake? Je, haujajaa maumivu? Moyo Wake umo katika maumivu, na maumivu haya ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kuelewa wala kutambua.
2 Kwa sababu kila kitu Anachokumbana nacho, kukabiliana nacho, kusikia, kuona na kupitia vyote ni upotovu wa wanadamu, uovu, na uasi wao dhidi ya, na upinzani wa ukweli. Kila kitu kinachotoka kwa wanadamu ndicho chanzo cha mateso Yake. Hivi ni kusema kwa sababu kiini Chake halisi si sawa na wanadamu waliopotoka, kupotoka kwa wanadamu kunakuwa ndiko chanzo cha mateso Yake makuu. Wakati Mungu anapokuwa mwili, hakuna anayeweza kupatikana anayeweza kuwasiliana, anayeweza kuwa na mabadilishano haya na Mungu. Yale mambo ambayo watu huzungumza ambayo wanapenda, ambayo wanafuatilia na kutamani yote yanahusu dhambi, na yana mielekeo ya uovu. Wakati Mungu anapokabiliana na haya, haya si kama kisu katika moyo Wake? Akiwa Amekabiliwa na mambo haya, Anaweza kuwa na furaha katika moyo Wake? Anaweza kupata kitulizo? Wale wanaoishi na Yeye ni wanadamu waliojaa uasi na uovu—je, moyo Wake utakosaje kuteseka?
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili