867 Mungu ni Msaada wa Milele wa Mwanadamu
1 Ingawa Bwana Yesu alifufuliwa, moyo Wake na kazi Yake vyote havikuwa vimeondoka kwa wanadamu. Aliwaambia watu Alipoonekana ya kwamba haijalishi ni umbo gani Alilokuwemo ndani, Angeandamana na watu, kutembea na wao, na kuwa na wao siku zote na katika sehemu zote. Na nyakati zote na mahali popote, Angewatosheleza wanadamu na kuwachunga, kuwaruhusu kumgusa na kumwona Yeye, na kuhakikisha kwamba hawatawahi kuhisi tena kama wasio na msaada. Bwana Yesu alitaka pia watu wajue yafuatayo: Maisha yao ulimwenguni hawapo pekee. Mwanadamu ana utunzaji wa Mungu, Mungu yuko pamoja nao; watu siku zote wanaweza kumwegemea Mungu; Yeye ndiye familia ya kila mmoja wa wafuasi Wake. Akiwa na Mungu wa kumwegemea, mwanadamu hatawahi tena kuwa mpweke au bila usaidizi, na wale wanaomkubali kama sadaka yao ya dhambi hawataishia katika dhambi tena.
2 Katika macho ya binadamu, sehemu hizi za kazi Zake ambazo Bwana Yesu alitekeleza baada ya kufufuka Kwake zilikuwa chache mno lakini Ninavyoona Mimi, kila kitu kilikuwa na maana yenye thamani sana na zote zilikuwa zenye umuhimu na uzito. Ingawa muda wa Bwana Yesu kufanya kazi katika mwili ulijaa ugumu na mateso, kupitia katika kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa mwili na damu, Alikamilisha vyema na kwa njia timilifu kazi Yake ya wakati huo akiwa kwa mwili ili kuwakomboa wanadamu. Aliianza huduma Yake kwa kugeuka mwili na Alihitimisha huduma Yake kwa kujitokeza kwa wanadamu Akiwa katika umbo Lake la mwili. Alikuwa mjumbe wa Enzi ya Neema, Aliianzisha Enzi ya Neema kupitia kwa utambulisho Wake kama Kristo. Kupitia utambulisho Wake kama Kristo, Alitekeleza kazi katika Enzi ya Neema na Akaipatia nguvu na kuwaongoza wafuasi katika Enzi ya Neema.
3 Inaweza kusemwa kuhusu kazi ya Mungu kwamba kwa kweli Yeye humaliza kazi Anayoianza. Kunazo hatua na mpango, na umejaa hekima ya Mungu, kudura Yake, na matendo Yake ya ajabu. Umejaa pia upendo na rehema za Mungu. Bila shaka, uzi mkuu unaotiririka katika kazi yote ya Mungu ni utunzaji Wake kwa binadamu; umejawa na hisia Zake za kujali ambazo Hawezi kuweka pembeni. Katika kila kitu ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake, kile kilichofichuliwa kilikuwa ni matumaini yasiyobadilika ya Mungu na kujali Kwake kwa wanadamu, pamoja na utunzaji wa Mungu wenye umakinifu na kuwathamini wanadamu. Mpaka sasa hakuna chochote kati ya hivi vyote ambacho kimebadilika.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili