934 Mungu Ndiye Mtawala wa Vitu Vyote

1 Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote. Yaani, vitu vyote vipo machoni mwa Mungu na katika eneo Lake la ukaguzi. Je, wanadamu wanaweza kuona vitu vyote? Kile ambacho wanadamu huona kimewekewa mipaka—ni tu kile wanachoona mbele ya macho yao. Wanadamu hawawezi kuona sehemu zilizo juu sana, mbali sana na kina sana. Kile wanachoweza kuona ni kilicho mbele ya macho yao na katika mpaka wa uwezo wao wa kuona.

2 Hata kama wanadamu wanajua mpangilio wa misimu minne katika mwaka na mpangilio wa ukuaji wa vitu vyote, hawawezi kusimamia au kutawala vitu vyote. Kwa upande mwingine, vile Mungu aonavyo vitu vyote ni kama vile Mungu angeona mashine Aliyotengeneza binafsi. Angejua kila kijenzi vizuri kabisa. Kanuni zake ni zipi, mipangilio yake ni ipi, na kusudi lake ni lipi—Mungu anajua vitu hivi vyote wazi na dhahiri. Kwa hiyo Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu! Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo. Wanadamu wakichunguza kitu fulani kidogo ambacho Mungu alifanya, wangetumia maisha yao yote kukichunguza bila kupata matokeo yoyote ya kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 933 Mwanadamu Anapaswa Kuthamini Viumbe wa Mungu

Inayofuata: 935 Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp