548 Mungu Awapenda Wale Walio na Azimio

1 Tunapaswa kuwa na azimio moja: Haijalishi jinsi mazingira yalivyo makali au aina gani ya matatizo tunayokabiliwa nayo, haijalishi jinsi tulivyo dhaifu, jinsi tulivyo hasi, hatuwezi kupoteza imani kwa mabadiliko katika tabia, na hatuwezi kupoteza imani katika maneno ya Mungu. Mungu amewapa wanadamu ahadi, na wanadamu wanapaswa kuwa na azimio na uvumilivu wa kujitolea kuzifanya. Mungu hapendi waoga; Anapenda watu wenye azimio. Hata kama umeonyesha upotovu mkubwa, hata kama umepitia barabara nyingi zilizopinda, au hata ikiwa njiani umekuwa na makosa mengi au umemkataa Mungu—au kuna watu wengine ambao wanamkufuru Mungu mioyoni mwao au wanamlaumu Yeye, wana mgogoro naye—Mungu hatazami jambo hili. Mungu huangalia tu ikiwa siku moja mtu ataweza kubadilika au la.

2 Mungu anamwelewa kila mtu kama mama anavyomwelewa mtoto wake mwenyewe. Anaelewa matatizo ya kila mtu, udhaifu, pamoja na mahitaji yake. Hata zaidi, Anaelewa shida gani kila mtu atakabiliwa nazo katika mchakato wa kuingia katika mabadiliko, na aina zipi za udhaifu na kushindwa kutakaokea. Hili ni jambo ambalo Mungu anaelewa zaidi. Ndiyo maana inasemwa Mungu huona ndani ya vina vya mioyo ya watu. Haijalishi wewe ni dhaifu kiasi gani, mradi huliachi jina la Mungu, mradi humwachi Mungu au njia hii, daima utakuwa na fursa ya kufikia mabadiliko katika tabia. Na ikiwa tuna fursa ya kufikia mabadiliko katika tabia basi tuna matumaini ya kuendelea kwetu kuishi. Ikiwa tuna matumaini ya kuendelea kwetu kuishi, tuna matumaini ya kuokolewa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Nini Maana ya Mabadiliko Katika Tabia na Njia Kuelekea Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 547 Mungu Awaokoa Wale Wanaopenda Ukweli

Inayofuata: 549 Matatizo Yote Yanaweza Kutatuliwa kwa Kufuatilia Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp