932 Mungu Aliumba Mbingu, Dunia na Vitu Vyote Kwa Ajili ya Mwanadamu

1 Mungu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu na pia akafanya mazingira ya kuishi. Kwanza, hoja kuu tuliyoijadili katika hadithi ni mwingiliano wa mahusiano na hali ya kutegemeana ya vitu vyote. Chini ya kanuni hii, mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu yamelindwa, yanaendelea kuishi na kudumu; kwa sababu ya uwepo wa mazingira haya hai, mwanadamu anaweza akastawi na kuzaliana. Mungu anatumia kanuni hizi na sheria kulinda uhai na uwepo wa vitu vyote. Ni kwa njia hii ndipo Anavikimu vitu vyote na Anamkimu binadamu.

2 Mungu anaamuru sheria zinazoongoza uendeshaji wa vitu vyote; Anaamuru sheria zinazoongoza uwepo wa vitu vyote; Yeye hudhibiti vitu vyote, na huviweka kutiana nguvu na kutegemeana, ili visiangamie au kutoweka. Hivi tu ndivyo wanadamu wanaweza kuendela kuishi; ni hivyo tu ndivyo wanaweza kuishi chini ya mwongozo wa Mungu katika mazingira kama hayo. Mungu ndiye bwana wa sheria hizi za uendeshaji, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia.

3 Kila kitu ambacho ni hai, kila kitu ambacho kina uhai kipo chini ya utawala wa Mungu. Kilipewa uhai baada ya Mungu kukiumba; ni uhai uliotolewa kutoka kwa Mungu na unafuata sheria na njia Alizozitengeneza kwa ajili yake. Hii haihitaji kubadilishwa na mwanadamu, na haihitaji msaada kutoka kwa mwanadamu; hivi ndivyo Mungu anavyokimu vitu vyote. Mungu anatumia vitu vyote—vitu alivyoviumba—kudumisha makazi ya binadamu kwa ajili ya kuishi na kulinda makazi ya binadamu, na hivi ndivyo Anavyomkimu mwanadamu na anavyokimu vitu vyote.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 931 Matendo ya Ajabu ya Mungu Katika Kusimamia Vitu Vyote

Inayofuata: 933 Mwanadamu Anapaswa Kuthamini Viumbe wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp