834 Mungu Huwakamilisha Wale Wanaompenda kwa Dhati

1 Kundi la watu ambao Mungu anataka kupata sasa ni wale ambao wanajitahidi kushirikiana na Mungu, wanaoweza kuiheshimu kazi Yake, na wanaoamini kuwa maneno Anayonena Mungu ni ya kweli, wale wanaoweza kuweka mahitaji ya Mungu katika vitendo. Ni wale walio na uelewa wa kweli katika mioyo yao. Ni hao ndio wanaoweza kukamilishwa, na wale ambao bila shaka watatembea katika njia ya ukamilisho. Wale wasio na uelewa wa wazi wa kazi ya Mungu, wale wasiokula na kunywa neno la Mungu, wale wasiotilia maanani neno la Mungu, na wale wasio na upendo wowote kwa Mungu katika mioyo yao. Wale walio na shaka na Mungu mwenye mwili, wasio na uhakika juu Yake, wasioyachukulia maneno ya Mungu kwa uzito na ambao daima humdanganya Mungu ni watu wanaompinga Mungu na ni wa Shetani; hakuna njia ya kukamilisha watu kama hao.

2 Mungu anafanya kazi ndani ya wale wanaotafuta na kulithamini neno la Mungu. Kadri unavyolithamini neno la Mungu, ndivyo Roho wa Mungu atakavyofanya kazi zaidi ndani mwako. Kadri mtu anavyolithamini neno la Mungu, ndivyo nafasi yake ya kukamilishwa na Mungu inavyokuwa kubwa. Mungu anawakamilisha wale ambao wanampenda Yeye kwa kweli. Anawakamilisha wale ambao mioyo yao iko katika amani mbele Yake. Ukiithamini kazi yote ya Mungu, yaani, ukiuthamini mwanga wa Mungu, ukiuthamini uwepo wa Mungu, ukithamini kujali na kuwekwa kwa Mungu, ukithamini jinsi neno la Mungu linakuwa ukweli wako na utoaji wa maisha, unafuata zaidi moyo wa Mungu. Hakuna kitu muhimu zaidi kwa waumini kama kupokea kazi ya Mungu, kupata ukamilifu, na kuwa wanaofanya mapenzi ya Mungu. Hili ndilo lengo unalofaa kufuata.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Anawakamilisha Wale Wanaoupendeza Moyo Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 833 Mahitaji Ambayo Mtu Lazima Afikie ili Kukamilishwa

Inayofuata: 835 Mungu Huwakamilisha tu Wale Wanaompenda kwa Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp