835 Mungu Huwakamilisha tu Wale Wanaompenda kwa Kweli

1 Kama mtapenda kukamilishwa na Mungu, lazima mjifunze kupitia mambo yote na kupatiwa nuru katika yote mnayoyapitia. Kiwe kizuri au kibaya, unafaa kufaidi kutoka katika kitu hicho na hakifai kukufanya ukae tu. Haijalishi ni nini, unafaa kuweza kukitilia maanani kwa kusimama upande wa Mungu, na wala si kuchambua au kukisoma kutoka kwa mtazamo wa binadamu. Kama hivi ndivyo utakavyopitia mambo katika maisha yako, basi moyo wako utazidiwa na mizigo ya maisha yako; utaishi siku zote katika mwanga wa uso wa Mungu na hutaweza kupotoka kwa urahisi katika matendo yako. Binadamu wa aina hii ana matarajio makubwa. Kunazo fursa nyingi za kukamilishwa na Mungu. Yote haya yanategemea kama ni nyinyi ndinyi mnaompenda Mungu kwa kweli na kama mnalo azimio la kukamilishwa na Mungu, kupatwa na Mungu, na kupokea baraka na urithi Wake.

2 Haitakubalika kwenu kuwa na azimio tu. Lazima muwe na maarifa mengi, vinginevyo siku zote mtapotoka katika matendo yenu. Wamejiwekea mipaka ya kufurahia tu neema ya Mungu na wako radhi tu kupokea tulizo fulani la mwili kutoka Kwake. Hawako radhi kupokea ufunuo zaidi na wa kiwango cha juu zaidi, hali ambayo inaonyesha kwamba moyo wa binadamu ungali nje siku zote. Na huwa hajali masharti na makusudio Mungu ya katika kumkamilisha binadamu ni yapi. Kwa hivyo maisha ya wengi yangali machafu na yaliyooza, bila dalili zozote za mabadiliko. Akitenda bila ukweli au kujitolea, na akiishi tu kwa vile viwango vya chini zaidi vya maisha, akiendelea kuwepo tu bila kusudi lolote. Wachache ndio wanaotafuta kuingia ndani ya neno la Mungu katika mambo yote, huku wakifaidi mambo mengi ya kusitawisha, wakiwa wenye utajiri mkubwa zaidi katika nyumba ya Mungu siku hii, na wakipokea baraka zaidi za Mungu. Kama unatafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote na unaweza kurithi ahadi za Mungu hapa ulimwenguni, kama unatafuta kupatiwa nuru na Mungu katika mambo yote na huiruhusu miaka kuyoyoma tu huku ukiwa umezubaa, Ni kupitia kwa njia hii tu ndipo unastahili na unafaa kukamilishwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 834 Mungu Huwakamilisha Wale Wanaompenda kwa Dhati

Inayofuata: 836 Kile Ambacho Wale Ambao Wamekamilishwa Wanamiliki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp