461 Mungu Anaweka Matumaini Yake Kabisa katika Mwanadamu
Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona; anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye. Tangu Alipoanza kusimamia, Mungu amekuwa akisubiria binadamu kumpa moyo wake, kumwacha Mungu kuutakasa na kuufaa ipaswavyo, kumfanya yeye kumtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu, kumfanya yeye kumstahi Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu amewahi kutazamia mbele na kusubiria matokeo haya.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili