23 Mungu Atawala Katika Ufalme

1 Mimi Natawala katika ufalme, na zaidi ya hapo, Ninatawala katika ulimwengu mzima; Mimi ni Mfalme wa ufalme na pia Mkuu wa ulimwengu. Kutoka wakati huu na kuendelea, Nitawakusanya wote wasio wateule na Nitaanza kufanya kazi Yangu katika mataifa, Na Nitatangaza amri Yangu ya utawala kwa ulimwengu mzima, ili kwa mafanikio Niweze kuingia katika hatua ifuatayo ya Kazi Yangu. Mimi nitatumia kuadibu ili kueneza kazi Yangu katika Mataifa, ambayo ni kusema, Nitatumia nguvu dhidi ya wale wote walio watu wa Mataifa. Kwa kawaida, kazi hii itafanyika kwa wakati mmoja na ile Kazi Yangu miongoni mwa wale waliochaguliwa. Wakati watu Wangu wanatawala na kushika madaraka duniani ndio pia itakuwa siku ambayo watu wote duniani watakuwa wameshindwa, na zaidi ya hayo, utakuwa wakati Wangu wa mapumziko—na hapo tu ndipo Nitawaonekania wale walioshindwa.

2 Mimi huonekana kwa ufalme mtakatifu, na kujificha kutoka kwa nchi ya uchafu. Wote walioshindwa na kuwa watiifu mbele Yangu wana uwezo wa kuuona uso Wangu kwa macho yao wenyewe, na uwezo wa kusikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe. Hii ni baraka ya wale waliozaliwa katika siku za mwisho, hii ni baraka Niliyoamua kabla, na hii haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Wakati Ninafungua rasmi hati ya kukunjwa ndio wakati watu ulimwenguni kote wanaadibiwa, wakati watu wote duniani wanakabiliwa na majaribu, na ndicho kilele cha Kazi Yangu; watu wote wanaishi katika nchi bila mwanga, na watu wote wanaishi huku kukiwa na tishio la mazingira yao. Kwa sababu siku Yangu inakaribia kwa wanadamu wote, kwa sababu haionekani kuwa mbali, lakini iko mbele ya macho ya mwanadamu, ni nani asiyeweza kuwa na uoga kwa sababu ya jambo hili? Ni nani asiyekuwa na furaha katika hili? Mji mchafu wa Babeli hatimaye umefika mwisho wake; mwanadamu amekutana na dunia mpya kabisa, na mbingu na dunia zimebadilishwa na kufanywa mpya.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 29” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 22 Ufalme Unapodhihirika Duniani

Inayofuata: 24 Anayeachilia Ngurumo Saba

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp