492 Ushauri wa Mungu kwa Mwanadamu

1 Ninamsihi kila mtu kufunga mdomo kuhusu nadharia na kuzungumzia kitu ambacho ni halisi, kitu ambacho ni cha kweli na thabiti, kujifunza baadhi ya “sanaa za kisasa,” kusema kitu ambacho ni halisi, kuchangia uhalisi kiasi, na kuwa na roho ya kujitoa. Uukabili uhalisi unapozungumza; usijiingize katika mazungumzo yasiyokuwa na uhalisi na yaliyotiwa chumvi ili kuwafurahisha watu au wakae na kukustahi. Thamani yake ni nini? Kuna maana gani katika kuwafanya watu kukutendea kwa ukunjufu? Kuwa “stadi” kiasi katika usemi wako, tenda haki zaidi kiasi katika matendo yako, kuwa mwenye busara zaidi kiasi katika jinsi unavyoshughulikia vitu, kuwa mwenye vitendo zaidi kiasi katika kile unachosema, fikiri kuhusu kuleta manufaa kwa nyumba ya Mungu katika kila tendo, acha dhamiri yako unapokuwa na muhemuko, usilipize wema kwa chuki, au kutokuwa na shukrani kwa wema, na usiwe mnafiki, usije ukawa na “ushawishi mbaya.”

2 Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, yahusishe zaidi na uhalisi, na unapowasiliana, zungumza zaidi kuhusu mambo ya uhalisi. Usijikweze; Mungu hataridhishwa na hilo. Katika miingiliano yako na wengine, kuwa mstahimilivu zaidi, fanya mazoezi zaidi ya kukubali, kuwa mkarimu zaidi kiasi, na ujifunze kutoka kwa “roho ya waziri mkuu.” Unapokuwa na mawazo ambayo si mazuri, fanya mazoezi zaidi ya kuukana mwili zaidi. Unapofanya kazi, zungumza zaidi kuhusu njia halisi na usiwe na majivuno sana, vinginevyo kile unachosema hakitaweza kufikiwa na watu. Starehe kidogo, mchango zaidi—onyesha roho yako ya kujitolea isiyo ya ubinafsi. Fikirieni zaidi makusudi ya Mungu, sikilizeni dhamiri zenu zaidi, kuweni wenye kuzingatia zaidi, na msisahau jinsi ambavyo Mungu huwanenea kila siku kwa uvumilivu na kwa dhati. Omba zaidi na ufanye ushirika mara kwa mara. Usiendelee kuwa mtu aliyekanganyikiwa sana, bali onyesha busara zaidi na upate umaizi fulani. Mkono wa dhambi unaponyooka, urudishe nyuma na usiuache utandae zaidi. Mnachokipata kutoka kwa Mungu si chochote bali laana; kuweni waangalifu.

3 Acheni mioyo yenu iwe na huruma kwa wengine na siku zote msiwapige kwa silaha mkononi. Shirikini zaidi kuhusu maarifa ya ukweli na mzungumze zaidi kuhusu maisha, mkiwa na roho ya kuwasaidia wengine. Tendeni zaidi na kusema kidogo. Tieni mengi zaidi katika vitendo na kidogo katika utafiti na uchambuzi. Acheni mguswe zaidi na Roho Mtakatifu, na mpeni Mungu fursa zaidi ya kuwakamilisha. Ondoeni sifa zaidi za kibinadamu; bado mna sifa nyingi za kibinadamu za kufanya mambo na matendo na namna yenu ya juujuu ya kufanya bado ni ya kuwachukiza wengine: Ziondoeni hizi zaidi. Hali zenu za akili bado zinachukiza sana; tumieni muda zaidi kuzirekebisha. Bado mnawapa watu hadhi kuu; mpeni Mungu hadhi zaidi, na usiwe mtu usiyekuwa na akili. “Hekalu” limekuwa la Mungu daima na halipaswi kutwaliwa na watu. Kwa ufupi, sisitiza zaidi juu ya haki na kidogo katika mihemuko. Ni bora zaidi kuuondoa mwili. Zungumza zaidi kuhusu uhalisi na kidogo kuhusu maarifa; kilicho bora zaidi kuwa kimya na kutosema lolote. Zungumza zaidi juu ya njia ya kutenda na ufanyemajivuno kidogo zaidi yasiyo na thamani. Itakuwa bora zaidi kuanza kutenda sasa.

Umetoholewa kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 491 Maarifa Si Mbadala wa Uhalisi

Inayofuata: 493 Ungependa Kuwa Tunda la Kufurahiwa na Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp