1007 Mpangilio wa Mungu wa Hatima ya Mwanadamu

1 Kiwango ambacho mwanadamu anamhukumu mwanadamu kinatokana na tabia zake; aliye na mwenendo mzuri ni mtu mwenye haki, na aliye na mwenendo wa kuchukiza ni mwovu. Kiwango ambacho Mungu anamhukumu mwanadamu kinatokana na iwapo asili ya mtu inamtii Yeye; anayemtii Mungu ni mtu mwenye haki, na asiyemtii Mungu ni adui na mtu mwovu, bila kujali iwapo tabia ya mtu huyu ni nzuri ama mbaya, na bila kujali iwapo hotuba ya mtu huyu ni sahihi ama si sahihi. Watu wengine wanatamani kutumia matendo mazuri kupata hatima nzuri ya baadaye, na watu wengine wanataka kutumia hotuba nzuri kununua hatima nzuri. Watu wanaamini kimakosa kwamba Mungu anaamua matokeo ya mwanadamu kulingana na tabia ama hotuba yake, na kwa hivyo watu wengi watataka kutumia haya kupata fadhila ya muda mfupi kupitia udanganyifu.

2 Watu ambao baadaye watasalimika kupitia pumziko wote watakuwa wamevumilia siku ya dhiki na pia kumshuhudia Mungu; wote watakuwa watu ambao wamefanya jukumu lao na wana nia ya kumtii Mungu. Wanaotaka tu kutumia fursa kufanya huduma ili kuepuka kutenda ukweli hawataweza kubaki. Mungu ana viwango sahihi vya mipangilio ya matokeo ya kila mtu; Hafanyi tu maamuzi haya kulingana na maneno na mwenendo wa mtu, wala Hayafanyi kulingana na tabia zao wakati wa kipindi kimoja cha muda. Hakika Hatakuwa na huruma na mwenendo wowote mbaya wa mtu kwa sababu ya huduma ya mtu ya zamani kwa Mungu, wala Hatamnusuru mtu kutokana na kifo kwa sababu ya gharama kwa Mungu ya mara moja. Hakuna anayeweza kuepuka adhabu ya uovu wake, na hakuna anayeweza kuficha tabia zake mbovu na hivyo kuepuka adhabu ya maangamizi.

3 Kama watu wana uaminifu kwa Mungu waonapo baraka lakini wanapoteza uaminifu wao wasipoweza kuona baraka na mwishowe bado wasiweze kumshuhudia Mungu na bado wasiweze kufanya jukumu lao kama wapasavyo, hawa watu waliomhudumia Mungu wakati mmoja kwa uaminifu bado wataangamizwa. Kwa ufupi, watu waovu hawawezi kuishi milele, wala hawawezi kuingia rahani; watu wenye haki tu ndio mabwana wa pumziko. Baada ya binadamu kuingia katika njia sawa, watu watakuwa na maisha ya kawaida ya binadamu. Wote watafanya jukumu lao husika na kuwa waaminifu kabisa kwa Mungu. Watatoa kabisa kutotii kwao na tabia yao iliyopotoshwa, na wataishi kwa ajili ya Mungu na kwa sababu ya Mungu. Watakosa uasi na upinzani. Wataweza kabisa kumtii Mungu. Haya ndiyo maisha ya Mungu na mwanadamu na maisha ya ufalme, na ni maisha ya pumziko.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1006 Masharti Manne ya Mungu Kumkamilisha Mwanadamu

Inayofuata: 1008 Mungu Huamua Mwisho wa Wanadamu Kutegemeza kwaKama Wanamiliki Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp