904 Mamlaka ya Mungu ni Ishara ya Utambulisho Wake
1 Nguvu za Mungu zinaweza kuumba viumbe vya mfumo wowote ulio na uzima na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe hai vyote. Vilevile, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuzaana kwa amri ya Mungu, ambapo baadaye Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote hai, na hakutakuwa na kupotoka kokote, daima dawamu.
2 Hakuna mtu au kifaa kilicho na mambo haya; Muumba tu ndiye anayemiliki na aliye na nguvu kama hizo, na hivyo basi yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au hali halisi ya mamlaka haya, kila mojawapo linaweza tu kuhusishwa na Muumba kwa sababu ni ishara ya utambulisho na hali halisi ya kipekee ya Muumba; na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba, mbali na Muumba, hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka” Huu ni ufasiri wa mamlaka ya kipekee ya Muumba.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili