927 Mamlaka ya Mungu ni Sheria ya Mbingu Ambayo Shetani Hawezi Kuzidi

1 Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea wazi Shetani, na hivyo Shetani hajawahi thubutu kuvuka mipaka hiyo. Katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazotilia mkazo kwenye mamlaka Yeye. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote. Ingawa ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu.

2 Kwa miaka milioni, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kukanyaga juu ya alama. Ingawa ni mwenye kijicho, Shetani ni “mwerevu” zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maelekezo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba yanatokana na upekee na mamlaka ya Mungu ndiposa viumbe vyote vinabadilika na kuzalisha katika njia ya mpangilio, kwamba mwanadamu anaweza kuishi na kuongezeka kupitia ndani ya mkondo ulioanzishwa na Mungu, huku hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuuharibu mpango huu, na hakuna mtu au kifaa kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 925 Mungu Hamruhusu Shetani Kuwadhuru Wale Anaotaka Kuokoa kwa Kupenda

Inayofuata: 928 Ingawa Mwanadamu Amepotoshwa na Kudanganywa na Shetani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp