906 Mamlaka ya Mungu Hayapimiki
1 Mamlaka ya Mungu hayawakiwaki yakizima, hayaji yakienda, na hakuna mtu anayeweza kupima namna ambavyo mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, wakati Mungu anabariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutaruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za maisha zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanakoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au hata ni vipi ambavyo mageuzi makubwa yamekuwa makubwa katika harakati zao za kuishi kwenye mazingira yao—haya yote yanajulikana kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake.
2 Haijalishi ni muda upi umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kama vile ndio mwanzo yametamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutambua kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia, ahadi hii itakamilishwa, na kutambuliwa, na, zaidi, kukamilishwa kwake na kutambuliwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba upana wa mamlaka ya Mungu na nguvu vinatosha kudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili