44 Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu

1 Mimi huangalia chini juu ya mambo yote kutoka juu, na Ninatoa mamlaka juu ya mambo yote kutoka juu. Kwa njia iyo hiyo, Nimeutuma wokovu Wangu juu ya dunia. Kamwe hakuna wakati ambapo Mimi Sitazami, kutoka mahali Pangu pa siri, kila hatua ya binadamu, kila wanachosema na kutenda. Binadamu Kwangu wako wazi kabisa: Mimi Nawaona na kuwajua kila mmoja. Mahali hapo pa siri ni makaazi Yangu, na mbingu ndiyo kitanda ambamo Mimi hujilaza. Nguvu za shetani haziwezi kunifikia, kwa maana Mimi nimejawa na uadhama, haki na hukumu.

2 Nimetembea ulimwenguni kwa miguu Yangu, Nikinyoosha macho Yangu juu ya anga yake nzima, na Nimetembea miongoni mwa wanadamu wote, Nikionja ladha tamu, ya asidi, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu, lakini mwanadamu hakuwahi kweli kunitambua, wala hakuniona Nikitembea ng’ambo. Kwa sababu Nilikuwa kimya, na Sikutenda matendo yasiyo ya kawaida, kwa sababu ya hili hakuna yeyote aliyeniona kwa kweli. Mambo hayako sasa kama yalivyokuwa wakati mmoja: Naenda kufanya mambo ambayo, tangu mwanzo wa uumbaji, dunia haijawahi kuyaona, Naenda kusema Maneno ambayo, kupitia enzi nyingi, wanadamu hawajawahi kuyasikia, kwa sababu Nauliza kwamba binadamu wote waje kunijua katika mwili.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 5” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 43 Vitu Vyote Viko Mikononi Mwa Mungu

Inayofuata: 45 Mungu Yuko Mbinguni na Pia Duniani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp