943 Tabia ya Mungu ni Yenye Huruma, Upendo, Haki na Uadhama

1 Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa binadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya kimwili; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangesita kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia moja ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni dhana moja ya hali halisi ya hasira ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu.

2 Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Yeye husita kufichua huruma au upole wa upendo wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa huruma Yake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kwa muda mfupi, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira na adhama Yake, ambavyo binadamu hatakiwi kukosea, na pia ni maonyesho ya dhana moja ya tabia Yake ya haki.

3 Wakati watu wanashuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuiona uadhama Yake au kuhisi kutovumilia Kwake kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia binadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona kidogo upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huku ni kutovumilia kosa kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 942 Mungu ni Mwenye Huruma Kuu na Mwenye Ghadhabu Kubwa

Inayofuata: 944 Mungu Aendeleza Kuwepo kwa Mwanadamu kwa Tabia Yake ya Haki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp