134 Asili ya Mungu Haibadiliki

1 Lakini inaashiria kutobadilika kwa tabia ya Mungu na kiini Chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia.

2 Hapo mwanzo, tabia ya Mungu ilikuwa siri kwa mwanadamu, na kamwe Yeye hadharani hakumfichulia mwanadamu tabia yake, na mwanadamu hakuwa na ufahamu kuhusu Yeye, na hivyo hatua kwa hatua Alitumia kazi Yake kumfichulia mwanadamu tabia Yake, lakini hii haina maana kuwa tabia Yake inabadilika katika kila enzi. Sio kweli kuwa tabia ya Mungu kila wakati inabadilika kwa ajili mapenzi Yake daima hubadilika. Bali, kwa kuwa enzi za kazi Yake ni tofauti, asili ya tabia Yake kwa ujumla hufichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, ili mwanadamu aweze kumjua Yeye. Lakini hii si kwa njia yoyote ushahidi kuwa Mungu hapo awali hakuwa na tabia fulani na tabia Yake imebadilika hatua kwa hatua kwenye enzi zinazopita—ufahamu kama huo ni wenye kosa.

3 Mungu humfichulia mwanadamu tabia yake fulani ya asili, kile Alicho, kwa mujibu wa enzi zinazopita. Kazi ya enzi moja haiwezi kueleza tabia nzima ya Mungu. Na kwa hivyo, maneno haya “Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani” yanarejelea kazi yake, na maneno haya “Mungu habadiliki” kinarejelea kile ambacho Mungu anacho na alicho kiasili. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja.

Umetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 133 Mungu Hufanya Kazi Mpya katika Kila Enzi

Inayofuata: 135 Kazi ya Mungu ni Mpya Daima na si Nzee Kamwe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp