13 Utukufu wa Mungu Wang’aa Kutoka Mashariki

1 Ninapopita katika mbingu na nchi mpya tu ndipo Ninachukua sehemu nyingine ya utukufu Wangu na kuifichua kwanza katika nchi ya Kanaani, Nikisababisha nuru kuiangazia dunia nzima, iliyozama katika giza totoro la usiku, ili kuruhusu dunia nzima kuja kwa nuru hiyo. Wacha watu wote duniani kote waje kupata nguvu kutoka kwa nuru, kuruhusu utukufu Wangu uongezeke na kuonekana upya kwa kila taifa. Wacha binadamu wote utambue kwamba Nilikuja zamani katika ulimwengu wa wanadamu na Nilileta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki zamani; kwani utukufu Wangu unang’aa kutoka Mashariki, ambako uliletwa kutoka Enzi ya Neema hadi leo. Lakini Nilitokea Israeli na kutoka huko Nikawasili Mashariki.

2 Wakati nuru ya Mashariki inapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba Nilishatoka Israeli zamani na Nimeanza kuchomoza upya Mashariki. Niliwahi kushuka Israeli na baadaye Niliondoka kutoka huko, Siwezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine, kwa kuwa kazi Yangu inauongoza ulimwengu mzima na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii ndiyo sababu Nimeshuka Mashariki na kuwaletea watu wa Mashariki Kanaani. Ningependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani, na kwa hiyo Naendelea kutoa maneno Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu, hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi.

Umetoholewa kutoka katika “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 12 Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki

Inayofuata: 14 Mungu Ameonekana Mashariki mwa Dunia na Utukufu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp