463 Matumaini ya Mungu kwa Binadamu Hayajabadilika
1 Katika sadaka ya Ibrahimu ya Isaka, Mungu aliuona uaminifu na utiifu huu wa Ibrahimu, na Akaona kwamba alikuwa amestahimili jaribio la Mungu kwake yeye. Hata ingawaje Mungu aliukubali uaminifu na utiifu wake, bado hakustahili kuwa mwandani wa Mungu, wa kuwa mtu aliyemjua Mungu, na kumwelewa Mungu, na alifahamishwa kuhusu tabia ya Mungu; alikuwa mbali sana na kuwa na akili sawa na Mungu na vilevile kuweza kufanya mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, katika moyo Wake, Mungu alikuwa bado mpweke na mwenye wasiwasi. Kwa kadri Mungu alipokuwa mpweke na mwenye wasiwasi zaidi, ndipo Yeye alipohitaji zaidi kuendelea na usimamizi Wake haraka iwezekanavyo, na kuweza kuchagua na kulipata kundi la watu wa kukamilisha mpango Wake wa usimamizi na kutimiza mapenzi Yake haraka iwezekanavyo. Hili ndilo lilikuwa tamanio lenye hamu kubwa la Mungu, na limebakia vilevile kuanzia mwanzo kabisa hadi leo.
2 Tangu Alipomuumba binadamu hapo mwanzo, Mungu ametamani kuwa na kundi la washindi, kundi ambalo litatembea na Yeye na linaweza kuelewa, kujua na kufahamu tabia Yake. Mapenzi haya ya Mungu hayajawahi kubadilika. Haijalishi ni muda gani bado Atasubiria, haijalishi barabara iliyo mbele ni ngumu kiasi gani, hata malengo Anayoyatamani yawe mbali kiasi kipi, Mungu hajawahi kubadilisha au kukata tamaa katika matarajio Yake kuhusu binadamu.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili