1028 Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu

1 Kila kitendo ambacho Mungu hufanya kina hali Yake ya uenyezi ndani yake, na pia kina hali Yake ya utendaji. Uenyezi wa Mungu ni kiini Chake, lakini utendaji Wake pia unajumuisha upande mmoja wa kiini Chake; hali hizi mbili hazitenganishwi. Mungu kufanya matendo katika uhalisi ni hali Yake ya vitendo ikitekeleza kazi, na kwamba Anaweza kufanya kazi kwa njia hii ni hali Yake ya uenyezi. Kitu chochote ambacho Mungu hufanya kina hali hizo mbili za uenyezi Wake na utendaji Wake, na yote hutekelezwa kulingana na kiini Chake; ni maonyesho ya tabia Yake, na ni ufunuo wa kiini Chake na kile Alicho.

2 Uwezo wa Mungu wa kufanya kazi Yake kwa kweli na kwa vitendo, na kutakasa na kutatua upotovu wa binadamu kwa kuonyesha ukweli, na pia Yeye kuweza kuwaongoza watu moja kwa moja—mambo haya yanaonyesha upande Wake wa vitendo. Anaonyesha tabia Yake mwenyewe na kile Alicho, na kazi yoyote ambayo wanadamu hawawezi kufanya, Yeye anaweza kuifanya; upande Wake wenye uweza unaweza kuonekana kutokana na hili. Mungu ana mamlaka ya kufanya Asemacho kiwe, kufanya amri Zake zisimame imara, na kufanya Asemacho kifanywe. Mungu anapozungumza, uweza Wake unafichuliwa. Mungu hutawala vitu vyote, humfanya Shetani amtumikie, hupanga mazingira ili kuwajaribu na kuwasafisha watu, na kuzitakasa na kubadili tabia zao—haya yote ni maonyesho ya upande wa Mungu wenye uweza. Kiini cha Mungu ni chenye uweza na cha vitendo, na vipengele hivi viwili vinakamilishana. Kila kitu afanyacho Mungu ni onyesho la tabia Yake na ufunuo wa kile Alicho. Kile Alicho kinajumuisha uweza Wake, haki Yake, na uadhama Wake.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 1027 Mungu Huvumilia Aibu Kubwa Kuwaokoa Wanadamu

Inayofuata: 1029 Ni Mungu tu Ampendaye Mwanadamu Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki