698 Hukumu ya Mungu Hutupa Uzima

1 Kila neno la Mungu hugonga eneo letu moja la kufisha, likituwacha na uchungu na kujawa na hofu Yeye hufichua dhana zetu, mawazo yetu, na tabia zetu potovu. Kutoka kwa yale yote sisi husema na kutenda, hadi kwa kila wazo na fikra zetu, asili na kiini chetu kinafichuliwa katika maneno Yake, yakituweka katika hali ya hofu na kutetemeka na bila mahali pa kuficha aibu yetu. Mmoja baada ya mwingine, Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua sisi wenyewe, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa wazi katika dosari zetu mbaya na hata zaidi kushindwa kikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba, machoni Pake, hatuna sifa hata moja inayoweza kutuokoa, kwamba sisi ndio Shetani anayeishi.

2 Hukumu na kuadibu Kwake kwa kweli zimetusababisha kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake kosa la binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni waovu sana, wachafu sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu hivi, kujiondoa asili na kiini hiki haraka iwezekanavyo, na kuwacha kuwa waovu na wa kuchukiwa na Yeye. Hukumu na kuadibu Kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na tusiasi matayarisho na mipangilio Yake tena. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kuendelea kuwepo na zilituwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu….

3 Sisi ni kundi la watu wa kawaida tu, waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, wale waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na wale maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, lakini sasa tumeshindwa na Yeye. Kutoka kwa Mungu tumepokea uzima, njia ya uzima wa milele. Licha ya mahali ambapo tunaweza kuwa duniani, licha ya mateso na dhiki tunazovumilia, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu pekee! Upendo wa Mungu unaenea mbele kama maji ya chemichemi, na unapewa wewe, na mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu. Kama vile tu mwezi hufuata jua kwa kubadilishana bila mwisho, vile vile ndivyo kazi ya Mungu haikomi kamwe, na inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata nyayo za Mungu na kukubali hukumu Yake na kuadibu Kwake.

Umetoholewa kutoka katika “Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 697 Faida za Kumwamini Mungu wa Vitendo ni Kubwa

Inayofuata: 699 Kutoa Sadaka ya Thamani Sana kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp