633 Hukumu ya Mungu ni Upendo

1 Ni ushuhuda gani ambao mwanadamu hatimaye huwa nao kwa Mungu? Yeye hushuhudia kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba tabia yake ni haki, ghadhabu, kuadibu, na hukumu; mwanadamu hushuhudia kwa tabia yenye haki ya Mungu. Mungu hutumia hukumu Yake kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, Amekuwa Akimpenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu—lakini ni kiasi gani kiko ndani ya upendo Wake? Kuna hukumu, uadhama, ghadhabu, na laana. Ingawa Mungu alimlaani mwanadamu katika wakati uliopita, Hakumtupa mwanadamu kabisa ndani ya shimo la kuzimu, lakini Alitumia njia hiyo kuisafisha imani ya mwanadamu; Hakumuua mwanadamu, lakini alitenda ili kumfanya mwanadamu awe mkamilifu.

2 Kiini cha mwili ni kile ambacho ni cha Shetani—Mungu alikisema sahihi kabisa—lakini ukweli unaotekelezwa na Mungu haukamilishwi kufuatana na maneno Yake. Yeye hukulaani ili uweze kumpenda, na ili uweze kujua kiini cha mwili; Yeye hukuadibu ili uweze kuamshwa, kukuruhusu wewe ujue kasoro zilizo ndani yako, na kujua kutostahili kabisa kwa mwanadamu. Hivyo, laana za Mungu, hukumu Yake, na uadhama na ghadhabu Yake—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Yote ambayo Mungu anafanya leo, na tabia yenye haki ambayo Yeye huifanya kuwa wazi ndani yenu—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na huo ndio upendo wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 632 Jua ya Kwamba Kuadibu na Hukumu ya Mungu ni Upendo

Inayofuata: 634 Unalindwa Kwa Sababu Unaadibiwa na Kuhukumiwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp