888 Upendo wa Mungu kwa Wanadamu Hauna Mipaka

1 Kusudi la Mungu kusema mambo haya ni kuwabadilisha na kuwaokoa watu. Ni kwa kuzungumza tu kwa namna hii ndiyo Anaweza kupata matokeo mazuri kabisa. Unapaswa kuona kwamba nia njema za Mungu ni kwa ajili ya kuwaokoa watu na zote ni mfano halisi waupendo wa Mungu. Bila kujali kama unauangalia kwa mtazamo wa hekima katika kazi ya Mungu, kwa mtazamo wa hatua na mbinu katika kazi ya Mungu, au kwa mtazamo wa wakaa wa kazi au mipangilio na mipango Yake sahihi, chote kina upendo Wake. Watu wote wana upendo kwa wana na mabinti zao; ili watoto wao waweze kutembea katika njia sahihi, wote wameweka jitihada kubwa. Wanapogundua udhaifu wa watoto wao, wazazi wanahofia kwamba ikiwa watazungumza kwa sauti laini, watoto wao hawatasikia na hawataweza kubadilika, na wanahofia kwamba ikiwa watazungumza kwa ukali sana, wataumiza staha ya watoto wao, na watoto wao hawataweza kuvumilia. Hii yote inafanyika kutokana na upendo, na wanaiwekea kiwango kikubwa cha jitihada.

2 Nyinyi kama wana na mabinti, huenda mmepitia upendo wa wazazi wenu. Upendo hauhusu tu upole na kujali; hata zaidi, unahusu kuadibu vikali. Zaidi ya haya, kila kitu Mungu afanyacho kwa wanadamu kinafanywa kutokana na upendoYeye hutenda chini ya sharti la mwanzo la upendo, ndiyo sababu Yeye kufanya kadri ya uwezo Wake kuleta wokovu kwa wanadamu waliopotoka. Hawashughulikii watu kwa kutimiza wajibu tu; Yeye hufanya mipango sahihi na kuiendeleza hatua kwa hatua. Kwa kuzingatia wakati, eneo, toni ya sauti, mbinu ya kuzungumza, na kiwango cha jitihada Anachoweka..., inaweza kusemwa kwamba yote hii inafichua upendo Wake, na yote inaelezea vizuri kabisa kwamba upendo Wake kwa binadamu hauna mipaka na haupimiki.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 887 Mungu Humkimu Kila Mtu kwa Unyamavu

Inayofuata: 889 Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp