237 Uzuri wa Mungu Daima Uko Mawazoni Mwangu

1 Ee Mungu! U mnyenyekevu na Uliyejificha katika mwili, Unapitia shutuma na kukashifu kwa mwanadamu, Unastahimili fedheha yote, lakini Unaendelea kuonyesha ukweli ili kuwaokoa binadamu—Unamwaga damu ya moyo Wako kumpa mwanadamu upendo Wako wote. Maneno Yako yote ni ukweli na uzima, hututakasa na kutubadilisha kila siku. Tunapopitia maneno Yako, twaona upendo Wako mwingi sana. Ee Mungu! Uzuri Wako daima u mawazoni mwangu.

2 Ninapopitia hukumu Yako, nimeonja upendo Wako. Kila neno la hukumu Yako ni kama upanga mkali ukiipasua asili yangu kwamba sina mahali pa kujificha. Nimejaa tabia ya kishetani na sina ubinadamu. Mwishowe nimeona uso wangu wa kweli. Tabia Yako ya haki imefichuliwa kwangu; sasa najichukia na nimetubu kweli. Ee Mungu! Uzuri Wako daima u mawazoni mwangu.

3 Ni hukumu Yako ambayo imeniokoa, ukali wa maneno Yako unaficha makusudi Yako ya dhati, lakini ninaposhikilia fikira zangu sina utiifu hata kidogo. Najiacha katika kukata tamaa, kukuelewa vibaya na kulalamika dhidi Yako. Maneno Yako yamenifariji na kunitia moyo muda baada ya muda, yakiniruhusu niinuke kutoka katika uhasi na udhaifu. Nimeona jinsi tabia Yako ilivyo nzuri na karimu. Ee Mungu! Uzuri Wako daima u mawazoni mwangu.

4 Maneno Yako yananiongoza katika shida zote. Kukamatwa na wale pepo ni tishio la kila siku; ni Wewe unisaidiaye kufuta machozi yangu ya huzuni na usiku huu wenye uchungu hauchushi sana. Nikiwa na upendo Wako kama rafiki wangu imani yangu inakua zaidi. Kupitia majaribu na usafishaji nimekufa na kuzaliwa upya, nimeelewa ukweli na kutupa ushawishi wa Shetani. Ee Mungu! Uzuri Wako daima u mawazoni mwangu. Nitakupenda milele na kuwa karibu nawe daima.

Iliyotangulia: 236 Mwishowe Naishi Kwa Kudhihirisha Mfano wa Bibinadamu

Inayofuata: 238 Nimeona Jinsi Ukweli Ulivyo wa Thamani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp