294 Huruma ya Mungu Imemruhusu Mwanadamu Kusalia Hadi Leo

1 Wanadamu hawajawahi kuona hata mojawapo ya matendo Yangu, wala hawajawahi kusikia hata mojawapo ya matamshi Yangu. Hata kama angekuwa ameona, yeye angegundua nini? Na kama angenisikia Nikiongea, yeye angeelewa nini? Kotekote katika ulimwengu, binadamu wote hukaa chini ya upendo Wangu, huruma Yangu, lakini pia binadamu wote hukaa chini ya hukumu Yangu, na vivyo hivyo chini ya majaribio Yangu. Nimekuwa mwenye huruma na upendo kwa wanadamu, hata wakati watu wote walikuwa wamepotoshwa kwa kiwango fulani; Nimegawa kuadibu kwa wanadamu, hata wakati watu wote walinyenyekea mbele ya kiti Changu cha enzi. Lakini, yupo binadamu yeyote ambaye hayuko katikati ya mateso na usafishaji Niliotuma?

2 Ni watu wangapi wanapapasa kwenye giza kutafuta mwangaza, ni wangapi wanajitahidi kwa uchungu kupitia kwa majaribio yao? Ayubu alikuwa na imani, na hata hivyo, kwa hayo yote, hakuwa anajitafutia njia yake mwenyewe? Ingawa ninyi watu Wangu mnaweza kusimama imara katika majaribio, kunaye yeyote ambaye, bila kuongea kwa sauti, anaamini katika moyo wake? Je, si anaona ni afadhali kuongea kuhusu imani yake ilhali anaishuku moyoni mwake? Hakuna binadamu ambao wamesimama imara katika majaribio, ambao wanatoa utiifu wa kweli katika majaribio. Kama Singefunika uso Wangu ili kuepuka kuangalia dunia hii, jamii nzima ya binadamu ingeporomoka chini ya macho Yangu ya kuchoma, kwa maana Siulizi chochote kutoka kwa binadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 10” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 293 Mungu Anatarajia Kuwa Binadamu Wataweza Kuendelea Kuishi

Inayofuata: 295 Binadamu wa Asili Walikuwa Viumbe Wanaoishi Walio na Roho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp