857 Huruma ya Mungu kwa Wanadamu Haijawahi Kukoma

Kisha Yehova akasema, Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?

1 “Ile huruma ya Muumba” si kauli tupu tu, wala si ahadi isiyotimizika; ilikuwa na kanuni, mbinu na majukumu ya kimsingi. Yeye ni kweli na halisi, na hatumii uwongo au utapeli wowote, na kwa njia ii hii huruma Yake inawekewa binadamu katika kila wakati na enzi. Hata hivyo, hadi siku hii, mabadilishano ya mazungumzo ya Muumba na Yona ndiyo kauli moja, na ya kipekee ya matamshi yanayoelezea ni kwa nini Anaonyesha huruma kwa binadamu, jinsi Anavyoonyesha huruma kwa binadamu, ni vipi Alivyo na uvumilivu kwa binadamu na hisia Zake za kweli kuhusu binadamu.

2 Mazungumzo haya ya Yehova Mungu yenye uchache na uwazi yanaonyesha fikira Zake kamili kuhusu binadamu; ni maonyesho ya ukweli ya mtazamo wa moyo Wake kwa binadamu, na ni ushahidi thabiti wa kutoa Kwake kwingi kwa huruma juu ya binadamu. Huruma yake haipewi tu vizazi vya wazee wa binadamu; lakini pia imepewa wanachama wachanga zaidi wa binadamu, kama vile tu ambavyo imekuwa, kuanzia kizazi kimoja hadi kingine. Ingawaje hasira ya Mungu hushushwa mara kwa mara kwenye pembe fulani na enzi fulani za binadamu, huruma ya Mungu haijawahi kusita. Kupitia kwa huruma Yake, Yeye huongoza na kuelekeza kizazi kimoja cha uumbaji Wake hadi kingine, huruzuku na kukifaa kizazi kimoja cha uumbaji hadi kingine, kwa sababu hisia Zake za kweli kwa binadamu hazitawahi kubadilika.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 856 Sikitiko la Mungu kwa Binadamu

Inayofuata: 858 Hisia za Kweli za Muumba kwa Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp