856 Sikitiko la Mungu kwa Binadamu

Kifungu kifuatacho kimerekodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11: “Kisha Yehova akasema, Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?”

1 Kwa kiwango cha maana ya juu juu, watu wanaweza kufasiri neno “huruma” kwa njia tofauti: Kwanza, inamaanisha “kupenda na kulinda, kuhisi huruma kuhusu kitu fulani”; pili, inamaanisha “kupenda kwa dhati”; na hatimaye, inamaanisha “kutokuwa radhi kukiumiza kitu fulani na kutoweza kuvumilia kufanya hivyo.” Kwa ufupi, unaashiria yale mahaba na upendo wa dhati, pamoja na kutokuwa radhi kukata tamaa na kumwacha mtu au kitu; unamaanisha huruma ya Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Ingawaje Mungu alitumia neno linalotamkwa mara nyingi miongoni mwa binadamu, matumizi ya neno hili yanaweka wazi sauti ya moyo wa Mungu na mtazamo Wake kwa mwanadamu.

2 Huku mji wa Ninawi ukiwa umejaa watu waliopotoka, walio waovu, na wenye udhalimu kama wale wa Sodoma, kutubu kwao kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake na kuamua kutowaangamiza. Kwa sababu mwitikio wao kwa maneno na maagizo ya Mungu ulionyesha mtazamo uliokuwa na tofauti kavu na ule wa wananchi wa Sodoma, na kwa sababu ya utiifu wao wa dhati kwa Mungu na kutubu kwa uaminifu dhambi zao, pamoja na tabia yao ya kweli na dhati kwa hali zote, Mungu kwa mara nyingine alionyesha huruma Yake ya moyoni naye akaweza kuwapa.

3 Tuzo ya Mungu na huruma Yake kwa binadamu haiwezekani kwa yeyote yule kurudufu; hakuna mtu anayeweza kumiliki huruma au uvumilivu wa Mungu, wala hisia Zake za dhati kwa binadamu. Muumba pekee ndiye aliye na upole kwa wanadamu hawa. Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu rehema na huba. Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu. Vilevile, Muumba pekee ndiye anayeweza kumpa huruma mwanadamu huyu na kufurahia viumbe vyake vyote.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 855 Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu

Inayofuata: 857 Huruma ya Mungu kwa Wanadamu Haijawahi Kukoma

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp